Bw. Kennedy Angelo Kajuna na Bi. Siza Mkoma wakiwa katika nyuso za furaha mara baada ya kufunga pingu za maisha katika kanisa Katoriki la Mt. Petro na Paulo lililopo Kijenge, Arusha. leo tar. 9.2.2012. Sherehe za kuwapongeza zinazofanyia katika ukumbi wa Chuo cha Uhasibu jijini humo.
Maharusi wakiingia kanisani.
Maharusi wakiwa katika sura ya usikivu wakati misa ikiendelea.
Padre Zacharia Matilo wa Kanisa Katoriki la jijini Nairobi, Kenya akitoa mafundisho kabla ya kuwafungisha ndoa.
Padre Zacharia Matilo wa Kanisa Katoriki la jijini Nairobi, Kenya akiwafungisha pingu za maisha Bw. Kennedy Angelo Kajuna na Bi. Siza Mkoma. Harusi hiyo ilifanyika katika kanisa Katoriki la Mt. Petro na Paulo lililopo Kijenge, Arusha.
Bwana Harusi Kenny Angelo Kajuna akimvalisha pete mkewe Siza Mkoma.
Bibi Harusi Siza Mkoma akimvalisha pete mumewe Kennedy Angelo Kajuna.
Kanisani ibada ikiendelea.
Bwana Harusi Kennedy akipokea sakramenti takatifu.
Bi, Harusi Siza Mkoma akipokea sakramenti takatifu.
Bwana Harusi Kennedy akisaini cheti huku akishuhudiwa na Padre Zacharia Matilo (kulia) wa Kanisa Katoriki la jijini Nairobi, Kenya pamoja na mkewe Siza Mkoma na wasimamizi wao.
Bi. Harusi Siza Mkoma akisaini cheti mara baada ya kufunga pingu za maisha na Bw. Kennedy Angelo Kajuna, pembeni yake anayemshudia ni Padre Zacharia Matilo (kulia) wa Kanisa Katoriki la jijini Nairobi, Kenya pamoja na wasimamizi wao.
Wakisaini vyeti.
Padre Zacharia Matilo wa Kanisa Katoriki la jiji Nairob, Kenya akimuelekeza sehemu ya kusaini msimamizi wa maharusi hao.
Padre Zacharia Matilo wa Kanisa Katoriki la jijini Nairobi akiweka saini yake kukamilisha zoezi hilo.
Padre Zacharia Matilo wa Kanisa Katoriki la jiji Nairobi, Kenya akiwapongeza maharusi hao kabla kuwakabidhi cheti.
Baba wa Bwana harusi, Mzee Kilucha akimpongeza kijana wake.
Mama wa bwana harusi akiwapongeza watoto wake mara baada ya kufunga pingu za maisha.
Pongezi zikimiminika kwa maharusi hao.
Mama zake wadogo na bwana harusi nao  hawakuwa nyuma kutoa pongezi kwa Kijana wao pamoja na mwali wao.
Kaka wa Bwana Harusi, Bwana Cathbert Angelo Kajuna (Mmilikiwa wa Mtandao huu wa Kajunason Blog) akitoa pongezi zake kwa shemeji yake.

Wapambe nao wakitoa pongezi kwa maharusi.
Msimamizi wa maharusi akimpa pongezi Bibi Harusi Siza Mkoma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: