Rais wa Shirikisho  la wasanii Tanzania (TAFF) Simon Mwakifywamba akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kuelezea juu ya matayarisho ya tamasha lao linalotarajiwa kufanyika Januari 26 ndani ya Dar Live jijini Dar es Salaam. Pembeni  wasanii wenzake waliomsindikiza katika mkutano huo.
---
Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa kushirikiana na Vennedrick Tanzania Limeted imeandaa Tamasha maalum la kujadili changamoto za kimaendeleo katika shirikisho la tasnia kwa ujumla tarehe 26 Januari 2013 kuanzia saa 4 mpaka usiku mnene katika ukumbi wa Dar Live.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari, Rais wa Shirikisho hilo Mwakifywamba, alisema kuwa mpka sasa maandalizi ya Tamasha hilo yamekamilika kama yalivyokuwa yamepangwa.

Alisema kuwa burudani zitakazotolewa katika tamasha hilo ni kama zifuatazo, Vichekesho vitaongozwa na Masanja Mkandamizaji, Joti, Kitale, Kingwendu, Mkono wa Mkonole, Bingwa wa Rivas Alex wa Macheji, Matata, The Supa Star King Majuto.

Upande wa Show ya Sebene Maalum itatolewa toka kundi la Bongo Muvi Unity wakiwemo Ray, Dk Cheni, JB, Chuz, Steven Nyerere, Irene Uwoya, Wema Sepetu, Yobnesh a.k.a BATULI. Jack Wolper na wengine wengi.

Aliongeza kuwa Dansi la Ukweli toka kwa bendi ya Twanga Pepeta, huku watakaonogesha zaidi atakuwa Snura na Kundi lake, Shilole Classic, Vitalis Maende a.k.a Sumu ya Teja, Mrisho Mpoto, Hemed PHD, Bongo Fleva itaongozwa na Tunda Man pamoja na Afande Selle toka Morogoro, Wasanii wengine ni Dude, Shija, Mtunisi, Rado, Niva na Burudani kibao kutokan kwa wasanii wa Maigizo Tanzania.

Kiingilio katika Tamasha hilo ni TZS 2000 kwa watoto, 7000 na 15, 000/=
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: