Marehemu Judith Chikaka Mapunda enzi za uhai wake.


Mwili wa Judith Chikaka ukiwa umelazwa ndani ya Jeneza Pamoja na mwili wa marehemu Mtoto wake mchanga.
Marehemu Judith Chikaka alifariki siku ya Jumapili  ya tarehe 13/01/2012 katika Hospitali ya Mwananyamala wakati alipofikishwa hapo kwa ajili ya kujifungua, kwa bahati mbaya na mapenzi yake muumba alifariki kabla ya kujifungua.


Mume wa Marehemu Judith, Bwana Erasto Mapunda akiwa amembeba mtoto wake wa kwanza aliyezaa na mkewe.
 
Baba mzazi wa marehemu Judith, Mzee Chikaka
 
Mama mzazi wa marehemu Mama Chikaka sakiwana majonzi makubwa baada ya kumpoteza mtoto wake kipenzi
 

Padre kutoka Parokia ya Kigamboni akiendesha Ibada ya misa takatifu ya kumwombea Judith alale kwa amani. Ibada hiyo ilifanyika nyumbani kwa Marehemu Judith maeneo ya Kigamboni Kibada.
 
Baadhi ya viongozi wa CCM Temeke wakitoa rambi rambi zao.
 
Spika wa Bunge la wanafunzi wa chuo cha Ardhi akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
 
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bwana S. Nyambui akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanachama na chama chao kwa ujumla.
 
Mume wa marehemu Judith akiweka Shada la maua katika nyumba ya milele ya mkewe
 
Kushoto ni mwakilishi wa Familia ya marehemu akipokea rambi rambi kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa marehemu kutoka wizara ya Ardhi
 
Mwakilishi kutoka Wizara ya Ardhi upande wa michezo akitoa salamu zake kwa niaba ya wanamichezo wenzake.
 
 
Hii ndio nyuma ya milele ya marehemu Judith Chikaka Mapunda.
 
Marehemu Judith  alizikwa jana katika makaburi ya Kibada maeneo ya Kigamboni, ameacha Mume na Mtoto mmoja.
 
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEME MAHALI PEMA PEPONI.
AMIN.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

3 comments:

  1. Daah nimesikitika sana yani hadi tumbo la uzazi limenikata,Inauma sana kupoteza watu wawili kwa wakati mmoja, Mungu ampe nguvu mume wa marehemu.Mungu wabariki na kuwalinda wanawake wote wajawazito jamani mpk naogopa,Mungu tusaidie.

    ReplyDelete

  2. tulikupenda ila mungu kakupenda zaidi RIP CHIKAKA!

    ReplyDelete
  3. pumzika kwa aman mwanangu judith na mjukuu wangu,mungu ndiye muweza wa yote.amen

    ReplyDelete