Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiendesha Kikao cha Muungano, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Januari 14, 2013. Wa pili (kushoto) ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili (kulia) Ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samiah Suluhu na (kulia) ni Waziri wa nchi Ofsi ya Makamu wa pili wa Rais zanzibar, Mohamed Aboud. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Makamu wa pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, wakati Makamu alipokuwa akiendesha Kikao cha Muungano kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Januari 14, 2013. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Muungano, kilichofanyika leo Januari 14, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar. Picha na OMR
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula (kulia) Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Ngosi Mwihava (katikati) na Mkurugenzi wa Muungano, Rajab Baraka (kushoto) wakifuatilia vifungu katika machapisho ya kujadili masuala ya Muungano, wakati wa kikao cha Muungano, kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (hayupo pichani), kilichofanyika leo Januari 14, 2013, katika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar. Picha na OMR
Baadhi ya Mawaziri wakiwa ukumbini humo wakati wakifuatilia kikao hicho cha Muumgano kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (hayupo pichani), leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar. Picha na OMR
Toa Maoni Yako:
0 comments: