Habari zilizotufikia mpaka sasa hali ya Mtwara sasa si shwari, machafuko ya amani yamekithiri na maandamano ya kupinga mradi wa gesi kwenda Dar yanazidi kupamba moto. Milipuko ya mabomu ya kutawaya watu yametumika ipasavyo lakini polisi wamezidiwa na bado vurugu zinaendelea. Ofisi na biashara nyingi zimefungwa mjini pote... magari ya serikali yanachomwa moto, nyumba za Mbunge Bi. Hawa Ghasia zimechomwa moto, Mahakama ya Mwanzo imechomwa moto, ofisi za Chama Cha Mapinduzi za mtaa zinachomwa moto, na sasa Wilaya ya Masasi, Tandahimba na Newala nao wameanza kuandamana. 

Mpaka sasa halmashauri ya Masasi nayo imechomwa moto na mafaili yote na Komputa na magari zimeteketea, nyumba ya Anna Abdalah imechomwa moto, ofisi ya mali asili imechomwa moto na watu wanabeba mbao kama zao.

Na hivi punde Magereza ya Masasi imevunjwa na wafungwa wote wametoroka... huku nyumba ya Mbunge wao na Magari yake kuchomwa moto.

Na mdau wa Kajunason Blog, Emannuel Senni- Mtwara. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: