Bondia Selemani Galile kushoto akijifua na Mohamed Mosco wakati wa mazozi yake ya kujitahalisha kupambana na Mbwana Ally mpambano utakaofanyika Yombo Dovya katika ukumbi wa Lupingu Pub February 2.
Bondia Selemani Galile akifanya mazoezi ya kukaza misuri ya tumbo wakati wa maandalizi ya mbambano wake na Mbwana Ally utakaofanyika Yombo Dovya katika ukumbi wa Lupingu February 2. Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
---
Na Mwandishi Wetu
Bondia Selemani Galile yupo katika mazoezi ya maandalizi ya mpambano wake dhidi ya Mbwana Ally utakaofanyika February 2 katika ukumbi wa Lupinga Pub uliopo Yombo Dovya
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Galile amesema yupo fiti kwa mpambano huo kwani kwa sasa anasubiri siku ya siku tu ili aweze kufanikisha
Galile aliongeza kuwa siku hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa wakazi wa Yombo Dovya kupata burudani ya masumbwi itakayosindikizwa na mabondia chipukizi
Antony Mathias atapambana na Abuu Mtambwe huku Ramadhani Mkundi akioneshana kazi na Kassim Gamboo na Mohamedi Zungu kutoka Zanzibar atapambana na Mbena Rajabu wa Dar
Siku hiyo ya Mpambano kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi atasambaza DVD zake mpya ikiwemo ya Marvin Hagler vs John Mugabi na Manny Pacuiao va Emanuel Juan Marquize ambazo atasambaza kwa mara ya kwanza katika ukumbi huo DVD hizo zinazoelekeza mbinu na shelia za masumbwi zenye uwezo wa kuwajengea uwezo mabondia na mashabiki kujua sheria mbalimbali za Masumbwi.
Toa Maoni Yako:
0 comments: