Na Juhud Felix wa Kajunason blog, Karagwe.

Askari wawili wa jeshi la polisi wilayani Ngara wameuwawa katika kijiji cha Kasheshe kata ya Rugu wilayani Karagwe kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa meno saba ya tembo yenye uzito wa kilogramu 34 kutoka katani humo.

Askari hao wakiwa na gari aina ya Noha namba hazitambulika kutokana na gari hilo kuchomwa moto na wananchi wenye hasira, walitokea wilaya ya Ngara wakiwa na mpango na wa kununua meno hayo kutoka kwa watu ambao hawajajulikana kuwauzia meno hayo.

Wananchi walifunga barabara zote zinazotoka kijijini hapo na kufanikiwa kulikamata gari hilo, na kuanza kuwapa kipigo hadi maaskari wawili kufa hapo hapo na mmoja ambaye amejulikana kwa jina moja la Braightoni kufanikiwa kutoroka na kujiasalimisha kituo kidogo cha polisi Kyanyamisa akiwa na silaha.

Wananchi hao waliweza kuwashambulia watuhumiwa na kisha gari walilokuwa nalo kuteketezwa kwa moto jambo lililopelekea maaskari hao wawili kupoteza maisha.

Askari hao waliouwawa walijulikana kwa majina ya E1446 Sajenti Thomasi Magiro na E 8889 Koplo Damasi Kisheke wote kutoka katika kituo cha polisi cha wilaya ya Ngara, ambapo pia askari mwingine ambaye amejulikana kwa jina moja la Braighitoni aliweza kuwatoroka wananchi hao na kujisalimisha katika kituo cha polisi Kyanyamisa.

Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya Nyakahanga wilaya ya Karagwe Dr Andrew Cesari amedhibitisha kupokea miili ya marehemu hao na alisema kuwa uchunguzi wa kitabibu umebainisha kuwa vifo vya marehemu hao vilitokana na kipigo kikali kilichosababisha majeraha ya kuvuja damu nyingi na kupelekea mauti hayo.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera Philipo Kalangi amefika katika eneo la tukio na kuthibitisha kuwa waliouwawa ni askari amesema kuwa uchunguzi unaendelea wa kubaini shughuli ilikuwa imewaleta askari hao na chanzo cha vifo vyao pia amewataka wananchi kutojichukulia sheria mikononi kama ambavyo hapa anaeleza wakati akiongea na wananchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: