Mkurugenzi mtendaji wa Airtel Tanzania akifafanua jambo jinsi wateja wa Airtel watakavyofaidika na huduma ya punguzo la gharama za maongezi hadi senti 10 kwa sekunde.
 Meneja Masoko wa Airtel Tanzania Rwebugisa Mutahaba akifafanua jambo jinsi wateja wa airtel watakavyoweza kufurahia punguzo nafuu ya la senti10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili kuanzia leo.
Wataalamu wa Airtel kitengo cha masoko na Mawasiliano wakionyesha vipeperushi vitakavyotumiwa kuelimisha jamii juu ya punguzo hilo wakiwa kwenye bonge la pozi.
Baadhi ya wafanyakazi wa airtel wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa punguzo gharama za huduma ya kuongea yaa Airtel-airte hadi senti 10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili.
Mfanyakazi wa Airtel kitengo cha ugavi akielezea kufuruahishwa na punguzo la kupiga simu kwa senti 10 baada ya dakika ya pili wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo leo katikA ofisi za Airtel Dar.
---
* Wateja kufurahia punguzo la asilimia 70 kupiga simu Airtel kwenda Airtel
* Wateja wa Airtel kupiga simu kwa senti 10 tu kwa sekunde baada ya dakika mbili
* Hakuna kujiunga, kila mteja wa malipo kabla ameunganishwa kufurahia viwango hivyo.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea na dhamira yake ya kutoa mawasiliano nafuu nchini kwa kutangaza punguzo la gharama za kupiga simu kwa lengo la kutoa fulsa zaidi kwa wateja wa Airtel wa malipo ya kabla kuendelea kufurahia huduma za Airtel

Sasa wateja wa Airtel watatozwa senti 10 kwa sekunde baada ya dakika ya pili ya maongezi kwa kupiga simu Airtel kwa Airtel.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Bw Sam Ellangallor alisema" tumepunguza gharama zetu za kupiga simu kwa asilimia 70 ili kuendelela kutoa huduma za kisasa, rahis na za bei nafuu kuweza kukidhi mahitaji ya wateja wetu sasa kupiga simu Airtel kwenda Airtel ni kwa bei nafuu zaidi ambapo wateja wa Airtel watatozwa senti 10 kwa sekundi baada ya dakika mbili za awali pale watakapopiga simu Airtel kwenda Airtel. Hakuna sababu ya kushindwa kuwasiliana kwani Airtel inakuwezesha kuongea na familia na marafiki zako siku nzima bila kikomo kwa gharama nafuu ya senti 10 kwa sekunde"

"Tunafahamu huduma ya mawasiliano ni nyenzo kubwa kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wateja wetu, Hivyo ndio maana Airtel tunajitahidi sana kuwaletea wateja huduma zenye ubunifu wa hali ya juu ili kutoa unafuu wa mawasiliano zaidi.

Airtel bado tunaendlelea na mkakati wetu wa kupunguza gharama za mawasiliano ili kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma bora".aliongeza Elangallor.

Airtel hivi karibuni imepunguza gharama za kutuma sms kwa kupitia huduma yake ya SMS Kichizi ambapo ujumbe mfupi wa maneno kwenda mtandao wowote unatozwa shilingi moja mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi 125 tu.

Akitoa maelezo zaidi ya huduma hiyo ya ya punguzo la gharama za mawasiliano Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi Beatrice Singano Mallya "leo tumewawezesha wateja wake kuongea kwa senti 10 tu kwa sekundu na kutoa uhuru zaidi wa kuongea.Hakuna haja kwa mteja wa Airtel kujiunga na gharama hizi mpya nafuu, ukiwa unatumia Airtel tu moja kwa moja utakuwa umeunganishwa na huduma hii nafuu.

Akizungumza juu ya muda Mallya aliongeza hizi ni gharma za kudumu zitakazopatikana nchi nzima

Airtel Tanzania ni kampuni inayoongoza kwa kutoa huduma bora na nafuu kama Airtel money na huduma ya internet ya kasi ya 3.75G. Mwanzoni mwa mwaka huu Airtel imetoa punguzo la gharama za ujumbe mfupi (SMS) ijulikanayo kama SMS kichizi inayowawezesha wateja wakel kutuma kila SMS kwa shilingi 1 kwa siku
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: