Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza rasmi kutoa fomu za ushiriki wa msimu wa pili wa programu ya kuwawezesha wajasiriamali ifahamikayo kama “Safari Lager Wezeshwa”, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya TAPBDS inayoratibu mchakato mzima wa Safari Wezeshwa,Joseph Migunda na kulia ni Mratibu wa Safari Wezeshwa,Laurance Andrew.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) tovuti ya  programu ya kuwawezesha wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa” ambayo itatumika pia kwa watu wanaotaka kujisajili kupitia mitandao. Tovuti hiyo ni www.wezeshwa.co.tz.
Meneja wa bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza rasmi kutoa fomu za ushiriki wa msimu wa pili wa programu ya kuwawezesha wajasiriamali ifahamikayo kama “Safari Lager Wezeshwa”, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kampuni inayoratibu mchakato mzima wa Safari Wezeshwa,Joseph Migunda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa sifa na vigezo vya ushiriki wa msimu wa pili wa programu ya kuwawezesha wajasiriamali ya “Safari Lager Wezeshwa”,ambavyo alivitaja kuwa ni (1). Wawe wachapakazi hodari (2). Wawe Wanamiliki biashara binafsi ambazo ni halali (3). wawe na umri kati ya miaka 18 hadi 40 na (4). wawe na nia ya kukuza biashara zao ili ziweze kuwasaidia wao na jamii inayowazunguka.shughuli hii ilimefanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo akionyesha moja ya fomu za ushiriki wa program hiyo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: