Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu Mjini Lindi, hukwadau mbalimbali wa masuala ya mapambano yA ukimwi wakishiriki kwa kufanya maonyesho na kutoa elimu na maelezo mbalimbali yanayohusu mapambano ya ukimwi, Rais Pia ameshuhudia utiwaji saini wa msaada wa Dola za Kimarekani Milioni 308 kutoka mfuko wa Global Fund uliosainiwa kati ya Katibu katibu  wa Ofisi ya rais  Paniel Lyimo na Ramadhan Kijahkatikabu Mkuu Wizara ya Fedha  huku Mfuko wa Global Fund ukiwakilishwa na Christoph Benn Mkurugenzi wa mfuko huo
Christoph Benn Mkurugenzi wa mfuko Global Fund akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani iliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya wananchi wa mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika mjini Lindi leo . kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatuma Mrisho na kushoto ni  mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila
Rais Jakaya Kikwete akipokea maandamano ya wananchi wa mkoa wa Lindi wakati wa maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani iliyofanyika mjini Lindi leo . kutoka kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Hussein Mwinyi, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti Ukimwi TACAIDS na mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila
Rais Jakaya Kikwete akishuhudia Utiwaji wa Saini wa msaada wa dola za Kimarekani milioni 308 kwa ajili ya mapambano ya Ukimwi  nchini, mkataba huo umesainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais  Paniel Lyimo kushoto na Ramadhan Kijah katikati, kulia ni Christoph Benn mkurugenzi wa Mfuko wa Global Fund, waliosimama nyuma kushoto ni Mkewa Rasi Mama Salma Kikwete, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi na kulia ni Ursula Muller Mjumbe wa bodi ya The Global Fund,
Rais Jakaya Kikwete akiongozana na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiingia kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi tayari kwa kushiriki katika maadhimisho ya siku ya ukimwi Duniani ambayo yamefanyika mkoani Lindi kitaifa kutoka kulia ni Mkurugenzi wa TACAIDS Fatma Mrisho na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila
Rais Jakaya Kikwete akimuonyesha jambo Mkurugenzi wa tume ya kudhibiti Ukimwi Fatma Mrisho wakati alipotembelea mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mjini Lindi leo.
Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa  Bw.Rajab Mwenda afisa masoko wa Mpango wa damu Salama wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani mjini Lindi leo.
Baadhi ya viongozi wa Dini na waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika maadhimisho hayo wakifuatilia kwa karibu matukio yaliyokuwa yakiendelea katika maadhimisho hayo.
Waheshimiwa viongozi wa serikali na baadhi ya wabunge wakiwa katika maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi.
Mwakilishi wa mfuko wa bima ya Afya ya Jamii mjini Lindi NHIF Bi. Fortunata Raymond wa tatu kutoka kulia akiongoza maandamano ya wafanyakazi wa mfuko huo katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani.
Kikundi cha matarumbeta kikiongoza maandamano hayo yaliyokuwa yakipita mbele ya Rais kwenye uwanja wa Ilulu leo mjini Lindi.
Kikundi cha kuigiza kutoka mfuko wa bima ya afya ya Jamiii NHIF kikiwapa ujumbe wananchi wqa mkoa wa Lindikuhusu maambukizi ya ukimwi
Kikundi cha ngoza za asili kutoka mkoani Lindi kkitumuiza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi
Mhashamu Baba Askofu Bruno Ngonyani wa Jimbo Katoliki Lindi akifanya maombi rasmi kwa ajili ya kuwakumbuka waliokufa kwa ugonjwa wa ukimwi na kuliombea taifa na wananchi wake kuepuka ugonjwa wa ukimwi na mapambano dhidi ya Ukimwi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: