Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Charles Kenyela (pichani)
akitoa taarifa ya msako wa kupambana na wahalifu kuelekea sikukuu za
mwisho wa mwaka na kusema jeshi la polisi mkoa wa Kinondoni limefanikiwa
kukamata wahalifu wa makosa mbalimbali na vielelezo kadhaa.
Alisema
wamewakamata watuhumiwa watano wanajihusisha na biashara ya kujiuza
kimwili na utali au wizi kwa wateja wao ambapo walikutwa na vidonge vya
aina mbalimbali pamoja na unga uliosagwa vyote vikidhaniwa kuwa ni
madawa ya kulevya ambayo hutumia kuwawekea wateja wao.
Aliwataja majina yao ni; Magreth Temu (33) mkazi wa Mwananyamala B, Nadra Fatii (30) Mkazi wa Mwananyamala Garden, Rosemary John (33) mkazi wa Mwananyamala Mwinjuma, Rahel John (31) na Lesa Jonathan wote wakazi wa Mwananyamala Shule.
Katika
msako huo wamekamatwa watuhumiwa 17 wanaojihusisha na biashara ya
bhangi, gongo, kamari na kubugudhi abiria huku vielelezo vilivyokamatwa
ni bhangi kilo moja na nusu na puli 300, gongo lita 35 na kete 20 za
madawa ya kulevya yanayodhaniwa kuwa ni Heroen.
Msako huo ndani ya saa 24 umemkamata mtu mmoja aitwaye Haji Juma mwenye umri wa miaka 32 mkazi wa Kawe Ukwamani akiwa na silaha Bastola aina ya Browning No. A 080416 iliyotengenezwa Czechlovakia.
Aidha Kamanda Kenyela amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni linaendelea na Operesheni zake kwa njia ya misako na doria ili kuwabaini madereva wa magari na pikipiki ambao wanakiuka Sheria za Usalama Barabarani na kusababisha ajali mbalimbali.
Kati ya kipindi cha mwezi Novemba hadi Desemba jumla ya magari na pikipiki 2,339 yalikamatwa kwa makosa mbalimbali ya usalama barabarani ambapo madereva walitozwa faini za hapo kwa papo (Notification) zilizofikia Shilingi 81,390,000/= na magari mengine 20 yalitozwa faini na SUMATRA ya jumla zaidi ya Shilingi 5,000,000/=.
Toa Maoni Yako:
0 comments: