Mambo makubwa yamefanyika katika uwanja wa CCM Kirumba usiku huu  jijini Mwanza ambapo Mwanamuziki Gwiji la miondoko ya bolingo, Barani Afrika kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Kofii Olomide akiwa na kundi lake amepagawisha mashabiki wa muziki wake katika tamasha la Tusker Carnival .

Mwanamuziki Kofii Olomide amefanya mambo makubwa kama alivyoshusha burudani jana kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam, Watu mbalimbali wamiminika kwenye uwanja wa CCM Kirumba ili kumuona mwanamuziki huyo (pichani juu) akiwa na first lady wa bendi hiyo mwanamama Cindy aliyetambulishwa kwa mashabiki wa jijini Mwanza.
 
Kofii Olomide akiimba huku akiwa amezungukwa na wanenguaji wake
Mwanamuziki Kofii Olomide akipanda jukwaani huku akisinddikizwa na waimbaji wake.
 
Mwanamuziki Cindy katikati Mwimbaji mahili wa mwanamuziki Kofii Olomide akiimba jukwaani kalba ya Kofii kupanda jukwaani.
 
Kazi iko hapa kama wanavyoonekana wanenguaji hao wakicheza kwa staili mpya.
 
Hii ilichezwa kwa kwenda mbele na kurudi nyuma huku wakiwa wameshikana.
 
Palikuwa hapatoshi kwa shoo kabambe.
 
Ili mradi burudani iliyopangika kutoka kwa wanenguaji hao
 
Ilichezwa kwa hisia pia
 
Kutoka kulia ni Ephraim Mafuru, Anitha Msangi Maurice Njowoka na Patrick Kisaka kutoka kampuni ya bia ya Serengeti wakishoo love kwa picha.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuru kulia ni Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga wakiwa katika picha ya pamoja
 
Wadau kutoka Miss Tanzania wakiwa katika onesho hilo.
 
Rachel wa THT akicheza na mmoja wa wanenguaji wa mwanamuziki Kofii Olomide.
 
Kofii Olomide akimpongeza msanii Rachel wa THT baada ya kuonyesha uwezo wake katika kuimba kwenye onesho hilo.
Waimbaji wa mwanamuziki Kofii Olomide wakiimba kwa hisia katika enesho hilo.
 
Rapa wa mwanamuziki Kofoo Olomide anayejulikana kwa jina la Computar akighani jukwaani huku wanenguaji wa kiume wakiingia jukwaani.
Jukwaani ni Recho wa kundi la  THT kutoka jijini Dar es salaam akinendelea kutoa burudani jukwaani
 H. Baba akifanya vitu vyake mbelea ya mashabiki wa jijini Mwanza wakati aktoa burudani ya utangulizi kabla ya mwanamuziki Kofii Olomide Kupanda jukwaani.
 
Pepe Kale wa Mwanza naye akaifanya mambo makubwa na kukubalika na umati wa mashabiki waliohudhuria katika onesho hilo.
Wasanii wa Kundi la THT likitumbuiza katika onesho hilo.
Bendi ya Hill Way ya Mwanza ikitumbuiza katika utangulizi
Kundi la Hill Way Band likifanya vitu vyake jukwaani katika utanguliziwa urudani za tamasha la Tusker Carnival kabla ya mwanamuziki Kofii Olomide kupanda jukwaani.
Mashabiki wakiwa wameanza kumiminika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mashabiki wakiwa  kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakisubiri kuona burudani ya Kofii Olomide.
Haya ni maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kujipatia bia yako ya Tusker Lager na vinywaji vingine vinavyotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
Haya ni maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya kujipatia bia yako ya Tusker Lager na vinywaji vingine vinavyotengenezwa na Kampuni ya bia ya Serengeti. PICHA ZOTE KWA HISANI YA FULLSHANGE.COM
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: