Yule mkali ambaye wengi walitarajia ndio atachukua mzigo wa milioni 50, Wababa Mtuka, anaachia kibao chake kipya kiitwacho ‘MY WIFE’ ambacho kakirekodia Surround Sound Studios chini ya mtayarishaji EMA the Boy.
Wababa, ambaye alitoa ushindani mkali kwa Walter na Salma, amesema anaamini wimbo huo utakuwa mkali na utashika sana wapenda burudani hapa nchini.
‘Nimetoa wimbo huu kama zawadi ya sikukuu kwa mashabiki wangu wote ambao wamenisapoti kipindi chote cha mashindano, lakini pia shukrani za pekee ziende kwa Zantel kwa kunirekodia wimbo huu’ alisema Wababa.
Wimbo huo, ambao ndio wa kwanza kutambulishwa kati ya nyimbo zote za washiriki wa Epiq BSS, umedhaminiwa na kampuni ya Zantel kama ahadi yake ya kuwarekodia bure wasanii waliongia 12 bora ya Epiq BSS.
Nyimbo nyingine za washiriki wa Epiq BSS zitaachiwa mwishoni mwa wiki hii.
Toa Maoni Yako:
0 comments: