Sajuki akipumzika kwa muda baada ya kuanguka.
Akitelemshwa toka jukwaani
HALI ya msanii wa filamu nchini, Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani kwa kuishiwa nguvu wakati alipopanda jukwaani kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama.
Tukio hilo lilitokea Jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.
Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh" na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake.
Wasanii wenzie walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi.
Akihojiwa muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi. ”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi
Toa Maoni Yako:
0 comments: