Baadhi ya watoto wanaoshambuliwa na ugonjwa wa funza. Kuanzia mtoto wa pili kutoka kulia ni miongoni mwa familia zinazoshambuliwa na ugonjwa wa funza eneo la Kibaoni Korogwe Vijijini.
Hata hivyo si watoto wa familia zote wamekubwa na ugonjwa huo, wapo ambao wanaangaliwa kwa karibu na familia zao kama wanavyoonekana baadhi ya watoto katika picha hii.
  Hapa mdau Mkuu wa Thehabari.com (kulia) akipata picha ya kumbukumbu na watoto katika eneo la Kibaoni Koogwe Vijijini juzi.
---
Na Mwandishi wa Thehabari Korogwe Vijijini

BAADHI ya watoto wanaokosa uangalizi wa karibu kutoka kwa wazazi au walezi wao wamekubwa na ugonjwa wa kushambuliwa na funza kwa kiasi kikubwa miguuni na mikononi hali iliyosababisha kuharibika kwa miguu yao na mikono kiasi kikubwa.

Idadi kubwa ya watoto walioathiriwa na wadudu hao wameonekana katika eneo la Kibaoni Korogwe vijijini, ambapo baadhi walipohojiwa na Thehabari walizitupia lawama familia zao kwa kutowaangalia kwa karibu kiasi cha kushambuliwa na funza. Kassim (si jina lake sahihi) anasema nyumbani kwao watoto wote wameshambuliwa na funza kuanzia miguuni hadi mikononi hali ambayo imewanyima kuwa huru katika kujumuika na wenzao.

“Wadudu hawa wanawasha na kuleta maumivu makali kiasi ambacho hushindwa hata kujumuika nawenzako…huwa najaribu wapunguza na kumsaidia mdogo wangu pia lakini wanatuzidi ni wengi,” anasema mtoto huyo. Hata hivyo mbali na maumivu na kuwashwa mfululizo, mikono ya kijana huyu imeshambuliwa vibaya na funza kiasi kinachomnyima uhuru wa kuitumia mikono vizuri kushikia vitu anuai kutokana na maumivu.

Ardhi ya kibaoni ni ya udogo mwekundu wenye vumbi hasa kipindi cha kiangazi. Baadhi ya watu wanasema wadudu aina ya funza wanaoshambulia binadamu ustawi zaidi katika mazingira machafu na yenye vumbi kiasi kikubwa. Watoto na hata watu wanaoshambuliwa na wadudu hao wanaishi katika mazingira kama hayo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: