Mwakilishi wa  NHIF na CHF Lindi Fortunata Kullaya akitoa elimu na  uhamasishaji kwa wanachuo wa chuo cha ualimu Nachingwea kufahamu umuhimu wa kujiunga na Mfuko. 
Mratibu wa CHF Wilaya ya Nachingwea Masiah Nyoni akifafanua maswali yaliyoulizwa kutoka kwa washiriki wa mafunzo ya elimu ya NHIF na Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) ambao ni  wanachuo wa chuo cha ualimu Nachingwea (NTTC).
Fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni yanayohusu changamoto na maboresho katika NHIF na CHF yalitolewa, pichani ni Ally Ngilima mwanachuo wa mwaka wa kwanza chuo cha ualimu Nachingwea akitoa maoni.
Veronika Luanda akipewa maelekezo na mwakilishi wa NHIF Lindi Fortunata Kullaya wakati wa utekelezaji wa mpango wa elimu kwa wanachama wa NHIF,uliofanyika  kwenye chuo cha Uuguzi Nachingwea (NTC).
Pichani ni mratibu wa NHIF/CHF Abinery Mkanya kwa chuo cha ualimu Nachingwea akiwasilisha majina ya wanachama waliojiunga papo kwa papo kwenye meza ya uratibu wakati wa zoezi la uhamasishaji. Na Paul Marenga NHIF - Lindi

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: