Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 usiku wa kuamkia ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi, mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar).
Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura.
Baadhi ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi.
 Washiriki wa EBSS 2012 wakiwa na washereheshaji wa shindano hilo.
 Washiriki wakiimba wimbo wa pamoja.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba akiimba pamoja na Shoma.
 Mshiriki akijieleza machache.
 Majaji wa Shindano la EBSS 2012, Master J, Madamu Ritha pamoja na  Salama Jabiri.
Mambo yalikuwa magumu mpaka ilibidi waletewe waone jinsi kura zinavyomiminika.
 Leyla Rashidi akimpa sapoti mshiriki wa EBSS 2012.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya mwenye hisia za pekee katika muziki, Linex
 Mshiriki wa shindano la EBSS Wababa akiwa msanii wa kizazi kipya Mwasiti.
 Walter akijimwaga jukwaani.
 Walter akiwa na Ditto.
Wasanii wa Muziki wa kizazi kipya, Amini na Barnaba wakijimwaga na wimbo wao mpya.
...ahaaaa...
...kuombana msamaha ilikuwepo...
Mashabiki wakijiachia.
Waandishi nao wakifuatilia kwa makini shindano hilo.
Ras Six akiwaga mambo.
 Mambo yote ya live yalisimamiwa na hao hapo.
 ... kila mmoja alijikakamua kuonyesha umahili wake wa kuimba.
 Salma nae hakuwa nyuma...
---
Mshiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 kutoka Dar es Salaam Walter Chilambo usiku wa kuamkia leo amekuwa mshindi na kujinyakulia kitita cha shilingi za Milioni 50 za Kitanzania.

Walter aliibuka kidedea mbele ya Salma Yusuf kutoka Zanzibar ambaye walifaikiwa kuingia naye pamoja fainali ya washiriki wawili tu kati ya watano ambao walianza fainali hiyo hapo awali. Walter ambaye dalili za ushindi wake zilianza kuonekana tangu awali mwa fainali hiyo ameweka historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kujinyakulia kitita kikubwa katika mashindano ya kusaka vipaji vya muziki.

Aidha katika shindano hilo mshiriki Walter pamoja na wenzake walipitia hatua tatu ambapo ya kwanza ilikuwa kuimba na msanii mmoja mmoja waliowachagua ambapo yeye aliimba na msanii Ditto kabla ya kuimba mwenyewe katika raundi mbili zilizofuata huku wakipigiwa kura na mashabiki katika raundi zote. Walter alitumia nyimbo moja ya Steve R n B “One Love”, na Nikikupata ya Ben Pol katika raundi zote mbili zilizofuata.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: