Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar imetoa
ushauri kwa Viongozi wa Jumuiya mbili za Kiislam Zanzibar wanaotuhumiwa
kwa makosa ya kuhatarisha usalama wa Taifa ya kutotendewa haki wakiwa
Gerezani wafungue kesi ya madai.
Ushauri
huo umetolewa na Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi
mara baada ya kupitia kwa makini maombi ya watuhumiwa hao yaliyofikishwa
mbele yake Novemba 8, mwaka huu kupitia kwa mawakili wa watuhumiwa hao.
Kesi
hiyo inawakabili watu wanane akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu
Zanzibar Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho
Sheikhe Mselem Ali Mselem.
Wengine
katika kesi hiyo ni Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan
Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar.
Akitoa
uwamuzi huo, Mh. Kazi amesema watuhumiwa wana haki ya kufungua kesi
mahakama kuu ya kile wanachokilalamikia na kwamba mahakama kuu itakuwa
na uwamuzi wa kuyasikiliza madai yao tofauti na kesi ya msingi kwa
watuhumiwa.
Kwa
kupitia kwa Mawakili wao, watuhumiwa hao walidai kuwa wananyimwa uhuru
na haki zao za msiki ikiwa ni pamoja na kupigwa marufuku yfugaji wa
ngevu wakiwa rumande chuo cha Mafunzo (magereza).
Watuhumiwa
hao wanakabiliwa na makosa mashta manne yakiwemo ya kutoa lugha za
uchochezi, kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa miundombinu ya
barabara mjini Zanzibar.
Wakizungumzia
kesi ya msingi kwa watuhumiwa hao, Waendesha Mashtaka wa Serikali
walidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamili na kwamba wanaomba siku
nyingine ya kutajwa.
Mrajisi huyo wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, ameiahirisha kesi hiyo hadi Alhamisi Novemba 29, mwaka huu itakapotajwa tena.
Kama
kawaida, Jeshi la Polisi lilifunga barabara zote za kuingia na kutoka
mahakamani na kuimarisha ulinzi ndani na nje ya mahakama hiyo ambapo
kila pembe walionekana Makachero wa Polisi na Askari wa Kikosi cha
Kutuliza Ghasia.
Nao
baadhi ya wananchi waliofika makahakamani hapo waliwataka waandishi wa
habari kuandika ukweli kuhusiana na kesi hiyo ili kuinusuru nchi yetu
kukumbwa na machafuko.
Watuhumiwa
hao wanatetewa na Mawakili wa kujitegemea Bw. Salum Toufik na Bw.
Abdallah Juma Kaka huku kwa upande wa Serikali ikiwakilishwa na Bw.
Ramadhani Nassibu na wenzake wawili kama Waendesha Mashtaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments: