Tanzania Mitindo House imefanya sherehe ya kusheherekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwa kula chakula cha mchana na watoto yatima kutoka ‘Malaika Orphanage Center’ na ‘Umraa Orphanage Center’ katika kituo chao cha kuchezea watoto yatima kilichopomanispaa ya Temeke.Pichani Juu na Chini ni Watoto wakicheza michezo mbalimbali katika sehemu maalum ya Tanzania MitindoHouse Fun Centre. Sherehe hizo zimedhaminiwa nan KIONDO COMMUNICATIONS INTERNATIONAL, AMAYA BEAUTY SALOON NA AIM GROUP.
Pichani Juu na Chini ni Watoto wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Tanzania Mitindo House (wenye sare za mashati ya Vitenge vinavyotengenezwa na kiwanda cha Morogoro Polytex kilicho chini ya Makampuni ya MeTL) wakisakata Kabumbu walipojumuika na watoto wenzao wa vituo vingine katika kusheherekea miaka 5 ya kituo chao.

Pichani Juu na Chini watoto wa kike nao walipata fursa ya kuchangamsha viungo kwa kucheza Netball katika kituo cha Mitindo House Fun Centre Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Jumping Castles lilikuwepo pia.
Mwenyekiti wa Kituo cha Tanzania Mitindo House (TMH) Bi. Khadija Mwanamboka akikata keki pamoja na Watoto wa kituo chake cha kulelea watoto yatima katika kusheherekea miaka 5 tangu kuanzishwa kwa kituo hicho ambacho mpaka sasa kina jumla ya watoto 10 saba wakiume na watatu wakike.
Mtoto Ashraf Kombo Mwanafunzi wa shule ya msingi ya Almuntazir alitumia fursa hiyo kusheherekea siku yake ya kuzaliwa na watoto yatima wa kituo cha Tanzania Mitindo House (TMH) kilichotimiza miaka 5 mwishoni mwa wiki.
Mama mzazi wa Ashraf akilimlisha keki mwanae mpendwa.
Mtoto Ashraf akimlisha keki mmoja wa watoto waliohudhuria sherehe hiyo.
Kwaito ilichezeka.
Na Kiduku pia.
Pichani juu na Chini ni Muda wa Msosi ulifika ni kitu cha Biriani tena.... Watoto wa ‘Malaika Orphanage Center’ , ‘Umraa Orphanage Center’ 'Tanzania Mitindo House' na walezi wao.
Mwenyekiti wa TMH Bi. Khadija Mwanamboka katika Picha ya pamoja na ugeni wake.


"Nyota Njema huonekana Alfajiri". Watoto wanaoelekea kuwa Wanamitindo wa baadae wakiweka pozi mbele ya Camera yetu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: