Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa ushirikiano
na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT) pamoja na Benki ya Posta Tanzania (TPB), inafurahi kutoa orodha
ya awamu ya tatu kwa waliopata viwanja. Orodha hii ni kwa maeneo ya
Ihungo, Rwome, Rwazi, Mugeza na Ijuganyondo.
Wote waliopata viwanja kwenye maeneo tajwa wanaombwa kuzingatia mambo
muhimu yafuatayo:
- Kukamilisha malipo ya kiwanja alichopata kupitia matawi ya Benki ya Posta:
Waliopata
viwanja watembelee tawi lolote jirani la Benki ya Posta Tanzania kukamilisha
malipo ya kiwanja (yaani Gharama halisi ya kiwanja kutoa gharama ya
dhamana iliyowekwa wakati wa kuomba kiwanja).
NB: Ikumbukwe
bei ya kiwanja inauzwa kwa mita ya mraba kama ifuatavyo:
ENEO
|
MATUMIZI
|
BEI KWA
MITA YA MRABA,Tshs
|
Rwome, Rwazi, Mugeza na Ijuganyondo
|
Makazi na maeneo ya kuabudia |
3,000
|
Biashara na Taasisi
|
3,300
| |
Ihungo
|
Makazi na maeneo ya kuabudia
|
3,400
|
Biashara na Taasisi
|
3,600
|
Kwa mfano, malipo ya kiwanja cha makazi cha Rwome, Rwazi, Mugeza na
Ijuganyondo chenye ukubwa wa 500m2 gharama inakokotolewa
kama ifuatavyo:-
(500m2 x 3,000) –
Dhamana. Kwa hiyo gharama yake itakuwa ni
1,500,000-200,000 = Tshs.1, 300,000
- Muda wa kukamilisha malipo:
Kila aliyepewa kiwanja atapaswa kufanya malipo haya katika benki ya Posta kuanzia
tarehe 01 Novemba, 2012 hadi 30 Novemba, 2012.
NB: Taarifa ya malipo (kwa atakayehitaji ufafanuzi zaidi)
inapatikana katika matawi ya Benki ya Posta au Halmashauri ya Manispaa
ya Bukoba kupitia simu 0689469965
- Stakabadhi ya malipo kutolewa na Benki ya Posta:
Baada ya kukamilisha malipo, tawi husika la Benki ya Posta litawajibika
kutoa stakabadhi ya malipo yenye mhuri wa Benki ya Posta.
- Kuoneshwa viwanja kwa waliopata viwanja:
Kwa wale waliofanikiwa kupata viwanja na kama watapenda kuoneshwa viwanja
vyao, watapaswa kufika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Idara ya Mipango
Miji kwa ajili ya kuoneshwa maeneo yao baada ya kukamilisha malipo.
Ratiba
ya kuoneshwa inapatikana Idara ya Mipango Miji na Ardhi Manispaa ya
Bukoba.
- Orodha ya watakaopata/watakaogawiwa viwanja awamu ya nne:
Zoezi la uchambuzi wa maombi mengine yaliyosalia kwa maeneo yote au pokelewa hadi tarehe 31 Octoba,2012
linaendelea. Orodha hii itatolewa kabla ya tarehe 30 Novemba 2012.
- Waliopata viwanja kwenye maeneo ya chaguo la pili:
Kutokana na kuwa na waombaji wengi wa viwanja kwenye baadhi ya maeneo, baadhi
ya waombaji imelazimika kuwapeleka katika maeneo ya chaguo lao la pili
au la tatu kama walivyobainisha katika fomu za maombi ya viwanja.
- Maandalizi ya Hati miliki ya kiwanja:
Hati miliki ya kiwanja itaandaliwa kwa wale ambao wamekamilisha malipo ya kiwanja.
Mara baada ya kukamilisha malipo ya kiwanja, kila aliyepata kiwanja
atapaswa kujaza tena majina yake kikamilifu, anwani na saini yake vitakavyotumika
kuandaa hati miliki ya kiwanja. Taarifa hizi zitajazwa kwenye fomu inayopatikana
benki ya Posta ambapo malipo yamefanyika.
Kama picha itatofautiana na ile iliyopo kwenye fomu ya maombi ya kiwanja,
aliyepata kiwanja atapaswa kufika ofisi za Manispaa ya Bukoba kutoa
uthibitisho wa mabadiliko hayo.
- Orodha ya waliopata viwanja katika maeneo tajwa hapo juu ni kama ifuatavyo:
Namba ya fomu
|
Jina la mwombaji
|
Eneo alilopata kiwanja
|
Kitalu (Block No)
|
Namba ya kiwanja
|
Ukubwa wa eneo
|
Orodha imetayarishwa kwa kufuata alphabeti za majina.
|
Tangazo hili linapatikana kwenye tovuti ya
UTT Tanzania na ya Mkoa wa Kagera pamoja na mtandao wa jamii wa Bukobawadau.
Muhimu:
- Wale wote waliopata viwanja katika awamu ya kwanza na ya pili yaani kwa maeneo ya Kagondo, Nyanga, Kyasha, Buhembe, Nshambya na Makongo muda wa kufanya malipo umeongezwa hadi tarehe 30 Novemba 2012 kutokana na maombi mengi ya waliopata viwanja.
- Wale watakaoshindwa kulipa kwa muda huo ulioongezwa Halmashauri itakuwa na hiari ya kugawa viwanja kwa watu wengine bila ya taarifa nyingine.
Karibu tuijenge upya Bukoba.
Hamisi Kaputa
MKURUGENZI WA MANISPAA
BUKOBA
Toa Maoni Yako:
0 comments: