IMG
9338 Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisalimiana na
Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Tanzania (TAA), wakati
alipofanya ziara katika Kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere jijini Dar
es Salaam Leo, kujionea shughuli Mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka
hiyo. Nyuma ya Waziri wa Uchukuzi ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,
Mhandisi. Suleiman Suleiman.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba(mwenye suti nyeusi)
akiangalia eneo la Kipunguni B ambalo lilifanyiwa tathmini kwa ajili
ya kuongeza eneo la Kiwanja cha Ndege cha Mwl. Julius Nyerere jijini
Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba akipata maelezo ya
namna kituo cha hali ya Hewa kinavyofanya kazi katika utoaji wa
Taarifa mbalimbali za hali ya Hewa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kutoka kwa Bi.
Pamela Gabriel kutoka Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA).Naibu
Waziri wa Uchukuzi alifanya Ziara hiyo kujionea shughuli mbalimbali
zinazofanywa katika Uwanja huo leo.
Naibu Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba akipata malezo
kutoka kwa Afisa kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA), Bw. Elieza
Mwalutende, wakati Naibu Waziri huyo alipotemmbelea Uwanja Wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwl . Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kujionea
shughuli mbalimbali zinazofanywa katika kiwanja hicho.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (aliyeweka mikono
miwili mfukoni) akipata maelezo ya namna kikosi cha zima Moto katika
Uwanja wa Ndege wa Mwl Julius Nyerere kinavyofanya kazi,Wakati wa
Ziara yake hii leo Katika uwanja Huo.
Waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba (aliyeweka mkono mfukoni)
akipata maelezo ya namna Genereta za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzani(TAA) zinavyofanywa kazi endapo umeme utakatika kutoka kwa Bi.
Rehema Ahmed (mwenye Hijabu), wakati wa Ziara yake katika uwanja huo
leo.
Hayo ni Majenereta yanayotumika endapo Umeme wa TANESCO
unapokatika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
jijjini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments: