Waziri wa Utalii wa Kenya Mh. Danson Mwazo katikati ambaye pia ni mwenyekiti wa mawaziri wa utalii katika nchi za Afrika Mashariki na Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania Balozi Khamis Kagasheki kulia, wakionyesha jarida la Round About East Africa la kwenye ndege. linaloelezea mambo mbalimbali ya utalii na pia kutangaza utalii wa nchi za Afrika Mashariki, mara baada ya kulizindua rasmi katika hafla iliyofanyika kwenye maonyesho ya dunia ya Utalii World Travel Market (WTM) Excel Jijini London nchini Uingereza, kulia ni Waziri wa Utalii wa Utalii wa Uganda pamoja na wawakilishi wa mawaziri wa utalii wa Rwanda na Burundi PICHA NA WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM
Mawaziri hao wa Utalii ktika nchi za Afrika Mashariki wakisaini jarida hilo kuashiria uzinduzi rasmi jijini London.
Waziri wa Utalii Kenya Mh. Danson Mwazo akizunguza katika hafla hiyo, katikati ni Mh. Jesca Eriyo Naibu Katibu Mkuu wa jumuiya Afrika ya Mashariki na Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili nchini Tanzania.
Mawaziri hao pamoja na wawakilishi kutoka Burundi na Rwanda wakionyesha jarida hilo mara baada ya uzinduzi rasmi.
Kikundi cha ngoma za Asili kutoka nchini Rwanda kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mh. Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na Mh. Balozi Ephraim Ngare wa Kenya wakijadiliana jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika maonyesho ya WTM Excel jijini London.
Baadhi wa wamiliki wa kampuni ya utalii ya Predators Safari Club kutoka Tanzania yaliyoshiriki maonyesha hayo wakiwa katika banda la Tanzania katitikati ni mkurugenzi wa kampuni hiyo Shabir Khan na mwenzake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: