Uongozi mpya wa Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) imeunda kamati nne maalumu kwa ajili ya maandalizi ya timu ya Taifa Stars inayojiandaa kwa mchezo wa kirafiki na timu ya Harambee Star ya Kenya unaotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza Novemba 14 mwaka huu.

Mwenyekiti wa MZFA Jackson Songora amesema kwamba kuundwa kwa kamati hizo kunafuatia chama hicho kupewa jukumu hilo na TFF Taifa kufanya maandalizi ya Kambi na mapokezi ili kuhakikisha timu ya Stars inacheza mchezo huo unaotarajiwa kufanyika katika dimba la CCM Kirumba siku ya Jumatano Jijini Mwanza kuendana na Kalenda ya FIFA inayoonyesha mchezo huo ni wa kirafiki wa Kimataifa.

Amezitaja Kamati hizo nne na wajumbe wake kuwa ni Kamati kuu nambapo itaongozwa na yeye mwenyekiti, Katibu ni Nasbu Mabrouk (Katibu wa MZFA), Mweka Hazina Jeremiah Tito Mahinya (Mweka hazina wa MZFA) na Mjumbe ni Almasi Moshi.

Kamati ya mapokezi na Usafiri itaongozwa na mwenyekiti wake  John Kadutu (Mwakilishi wa vilabu wa MZFA), Wajumbe ni Mohamed Kasanga na Munga Lupindo (Katibu wa NDFA) huku Kamati ya Matangazo, Habari na Uhamasishaji itakuwa na wajumbe wanne ambapo mwenyekiti wake ni Vedastus Lufano (Mjumbe wa Mkutano mkuu TFF wa MZFA), Katibu Albert G Sengo(Clouds FM Mwanza), Wajumbe ni Juma Msaka (Katibu wa IDFA) na Wessa Juma.

Mwenyekiti Songora ametoa wito kwa wadau na wapenda
soka kutoka Mkoa wa Mwanza na Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa kuunga mkono timu ya
Taifa Stars inayowasili kesho jioni (Jumapili) Novemba 11 mwaka huu  kwa kushiriki katika mapokezi ya timu hiyo
kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kuhakikisha wanaonyesha hamasa wakati
wakishuhudia mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa CCM Kirumba huku pia
akiwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi siku ya Jumatano kuishangilia na kushudia
mchezo huo kati ya Taifa Stars na Harambee Star ya Kenya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati ya Matangazo,
Habari na Uhamasishaji Vedastus Lufano amesema kwamba baada ya mchezo huo wa
jumatano timu hiyo ya Taifa Stars itaendelea na kambi jijini Mwanza kabla ya
timu hiyo kuelekea jijini Kampala kushiriki CECAFA Challeng Cup ambapo timu
mbalimbali za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zitashiriki.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: