Na Mohammed Mhina wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Kocha
mpya aliyetangazwa jana na ZFA, leo limetangaza kikosi kipya
kitakachoshiki katika michuano ya Challenge baadaye mwaka huu.
Kocha
huyo salim Bausi ambaye aliwahi kuzichezea timu kadhaa visiwani
Zanzibar, amewataja wachezaji 26 kutoka timu mbali,mbali zikiwemo
zinazoshiriki katika michuano ya Vodacom Tanzania Bara.
Waliotangazwa
kujiunga na kikosi cha Zanzibar Heros kwa nafasi ya ugolikipa ni
Mwadin Ali kutoka Azam Dar es Salaam, Suleiman Hamad Brek Sera Zanzibar
na Abdallah Juma kutoka timu ya Kipanga inayomilikiwa na JWTZ.
Katika
safu ya ulinzi Kocha huyo huyo amewataja Nasoro Masudi toka timu ya
Simba Dae es salaam, Samir Haji Nuhu toka Azam, Agrey Moris Azam, Nadiri
Haroub Kanavaro kutoka timu ya Yanga ya Dar es Salaam, Aziz Shaweli Ali
kutoka timu ya KMKM ya Zanzibar, Mohammed Juma Azan kutoka timu ya JKU
Zanzibar na Ali Mohammed Seif wa timu ya Mtende Ranges Zanzibar.
Wachezaji
wa kiungo ni Hamad Mshamata wa Timu ya Chuoni Zanzibar, Ali Bakari
Mtende Rangers Ishaka Mohammed wa JKU, Twaha Mohammed Mtibwa, Suleiman
Kasim Selembe wa timu ya Coast Union ya Tanga, Sabri Ali Makame wa timu
ya Zanzibar All Stars na Makame Gozi kutoka Timu ya Zimamoto na Uokoaji
Zanzibar.
Wingine
katika safu hiyo ya kiungo ni Issa Othman Ali wa timu ya Miembeni,
Zanzibar, Adeum Salehe wa timu ya Break Sela ya Zanzibar, Abraharim
Humudi na Hamissi Mcha Hamiss, kutoka katika timu ya Azam ya DSM.
Kocha
huyo amewataja wachezaji wa nafasi ya Ushambuliaji kuwa ni Amiri Hamad
JKT Oljoro Arusha, Jaku Juma Jaku wa Mafunzo, Abdallah Othuman wa
Jamhuri Pemba, na aliyemtaja kwa jina moja la Nassoro wa timu ya JKU
Unguja, na Faki Mwalim wa timu ya Chipukizi ya Pemba.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari mjini Zanzibar, Kocha huyo amesema kuwa amepania
timu yake kuchukua kombe la Challenge ili kukithi matakwa ya Rais wa
Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
Naye
Katibu Mkuu wa ZFA Kasim Haji, amewaomba wananchi wote wa Zanzibar
wakiwemo Wafanyakazi wa Mashirika mbalimbali ya Umma na wale wa Serikali
Zanzibar pamoja na Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi
kuisaidia titu hiyo kwa michango ya hali na mali.
Amesema
timu hiyo sio mali ya mtu mmoja ama ZFA peke yake, bali ni ya
Wazanzibar wote na hivyo hawanabudi kutoa michango yao ya hali na mali
ili kuiwezesha timu hiyo ya Taifa ya Zainzibar kutekeleza agizo la Rais
wa zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein aliyetaka kuimarishwa kwa timu hiyo
ili iweze kuleta kombe la Challenge mwaka huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments: