Balozi
wa kinywaji cha Hennessy, Cyrille Auriol, na Mwenyekiti wa Makampuni ya
Qweensway Group, Amin Hirjee, wakimzawadia DJ maarufu nchini, DJ Too
Short mkanda wa ushindi katika shindano la Hennessy DJ Challenge
lililofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa Serena Hotel, jijini Dar es
Salaam.
-wandishi Wetu
DJ Mohamed Ali maarufu kwa jina la “DJ Too Short” ameibuka mshindi katika shindano la Hannessy DJ Challenge lililofanyika kwenye ukumbi wa hotel ya Serena jijini.
Ushindi
wa DJ Too short umetokana na jinsi alivyoweza kuwachezesha mashabiki
kibao wa kinywaji cha Hennessy katika usiku maalum kinywaji hicho.
Balozi wa dunia wa Hennessy, Cyrille Auriol na Mwenyekiti wa makampuni ya Qweensway Group, Amin Hirjee walimzawadia zawadi ya ushindi DJ huyo.
Kutokana
na ushindi huo, DJ Too Short anakuwa Mtanzania wa kwanza kushinda
nafasi hiyo na kuzawadiwa mkanda wa utambulisho wake na yeye kushukuru
kwa mafanikio hayo.
Mbali
ya tukio hilo, Balozi Auriol alikutana na wadau mbali mbali wakiwemo
wafanyabiashara na wadau wa masuala ya maonyesho ya mavazi (modal) au
walimbwende na kujadili changamoto mbali mbali zinazowakabili hasa
wafanyabiashara wa vinywaji.
Balozi
huyo alifanya ziara yake ya siku mbili, ikiwa ni miongoni mwa ziara
yake ya siku tano katika nchi za Afrika Mashariki. Hii ni mara ya pili
kutembelea Tanzania.
Alisema
kuwa biashara ya vinywaji ambayo inawahusu wafanyabiashara, wanamuziki
na sekta nyingine kwa sasa inakuwa kwa kasi pamoja na kuwepo kwa
changamoto mbali mbali.
Alisema
kuwa wanajitahidi kuondoa changamoto hizo na nyingi zinatokana na
ushindani katika soko husika na moja ya mikakati yao ni kuwafundisha
watoa huduma hiyo ili kuweza kufikia kiwango cha kimataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: