Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Benki ya KCB nchini imeanza kutoa mafunzo kwa
wajasiliamali wadogo na wa kati ili kuwawezesha kukuza miradi na mitaji
yao ya kiuchumi.
Wakati
wa mafunzo hayo, pamoja na mambo mengine wakufunzi wa Benki hiyo
wamesema nia ni kuongezea uwelewa wa namna ya kuanzisha miradi kuendesha
biashara ndogondogo na utunzaji wa fedha benki kwa wajasiliamali hao.
Wakati
wa mafunzo hayo, pamoja na kuelimishwa masuala mbalimbali juu ya kukuza
mitajio na uansishaji wa biashara mpya, Wakufunzi Bw. Fredrick Lyimo na
Bw. Francis Mandala, wamesema benki hiyo inaendelea na mpango wake wa
kuboresha huduma kwa wateja.
Wamesema
kuwa pamoja na kutoa elimu hiyo kwa wajasiliamali, KCB Bank ambayo ina
matawi katika nchi zote tano za Afrika ya Mashariki, pia hutoa misaada
mbalimbali ikiwemo ya Vifaa vya Afya, Elimu na huduma nyingine za
kijamii.
Washiriki
hao wameelimishwa jinsi ya kuweza kuomba na kupatiwa mikopo pamoja na
kufundishwa jinsi ya kuitumia mikopo wanayoipata.
Akitoa
elimu juu ya biashara na namna ya kukuza mitaji, mmoja wa wakufunzi Bw.
Peace Lumelezi, amesema kuna haja ya kila mfanyabiashara kutofautisha
biashara yake naya mwingine ili kupata faida.
Amesema
kuwa hata kama biashara ya mfanyabiashara mmoja inafanana naya mwingine
katika eneo moja, lakini ni lazima kufanyabiashara makini atofautishe
biashara yake hata kwa lugha kwani wateja wanahitaji huduma bora.
Amewashauri
pia wafanyabiashara kutokwepa kodi za Serikali na kujiwekea bima ili
kuepuka ajali na hasara za majanga ya moto ama wizi.
Amewakumbusha
wajasiliamali hao mfanya biashara zao kwa kufuata taratibu na masharti
ya leseni zao na kuepuka kukwepa kodi mambo yanayoweza kupelekea
kufilisiwa ama kushitakiwa na Mamlaka ya Kodi za mapato yaani TRA kwa
upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ZRB kwa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Nao
baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, wameelezea changamoto mbalimbali
zinazowakuta na kusema baadhi ya waomba mikopo wamekuwa wakitoa taarifa
za uongo katika mabenki ili mradi waweze kupatiwa mikopo jambo ambalo
halijengi uaminifu kwa taasisi za fedha.
Pamoja
na kuelezea kunufaika na mafunzo hayo, washiriki hao pia wameiomba
benki ya KCB hapa nchi kuangalia uwezekano wa kuongeza matawi zaidi ya
kenki hiyo pamoja na kuongeza idadi za mashine za kutolea fedha yaani
ATM karibu na maeneo yenye wananchi wengi.
Wamesema
kwa ulimwengu wa sasa hakuna mtu anayependa kutembea na fedha nyingi
mfukoni kwa kutoka eneo moja hadi jingine kwa kuhofia kuporwa ama kuibwa
kwa fedha zake.
Wamesema
kama kutakuwa na matawi mengi ya benki ni rahisi kwa wajasiliamali
kufanya biashara zao na kuweka fedha zao benki lakini wakazichukua hata
kwa kupitia katika mashine za ATM pale wanapozihitaji kwa matumizi ya
kawaida ama ya kibiashara.
Hata
hivyo wamepongeza juhudi zinazochukuliwa na Benki hiyo katika
kuwaelimisha wajasiliamali bila kujali kama ni wateja wa benki hiyo ama
vinginevyo.
Wamesema elimu hiyo imewasaidia kwa kiasi kikubwa kujitambua na jinsi ya kukuza mitaji na kuboresha biashara zao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: