Balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na mikakati yake ya kufanya mazungumza na wafanya biashara mbali mbali wa hapa nchini.
Viongozi wa kinywaji cha Hennesy pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Waandishi wakiwa makini kufuatilia.
---
Na Mwandishi wetu
Balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, yupo nchini kwa ajili ya shughuli mbali mbali pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa jiji la Dar es Salaam.
Auriol aliwasili jijini juzi na kufanya mazungumza na wenyeji wake kabla ya kuelezea nia ya safari yake ambayo lengo kubwa ni kutanua soko la kinywaji hicho maarufu duniani kwa Watanzania nan chi za Afrika Mashariki.
Alisema kuwa pamoja na kukutana na wafanyabiashara, pia atakutana na watu wa sekta tofauti, miongoni mwao ni wanamuziki na wanamitindo. Ziara ya balozi huyo itakuwa ya siku tano.
Alifafanua kuwa ujio wake ni mara ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na ameona kuna mafanikio makubwa kwa wafanyabiashara na hasa katika soko la vinywaji vikali.
Alisema kuwa kinywaji cha Hennessy kwa sasa ndicho kinatamba katika ukanda huu na hivyo kuna haja kwa Watanzania kuanza kupartavradha kwa ajili ya kujenga mwili na afya bora. Ikiwa na zaidi ya historia ya miaka 250, Hennessy inatajwa kuwa kinywaji (Cognac) bora zaidi duniani.
Pia Auriol atakutana na wapenzi wa Hennessy katika matukio mbalimbali maalumu ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo baadhi ya wanawake watakaochaguliwa watapata fursa ya kujifunza historia ya kinywaji cha Hennessy lakini pia kuonja aina mbalimbali za kinywaji hicho lengo likiwa kuwafundisha wanawake namna ya kufurahia kinywaji hicho wakiwa majumbani mwao.
Balozi Auriol pia atahudhuria chakula cha jioni na wafanyabiashara wa hapa nchini katika mgahawa wa Akemi uliopo katika ghorofa la Diamond Jubilee. Balozi Auriol atatoa elimu kuhusu Hennessy ikifuatiwa na uonjaji wa kinywaji hicho pamoja na chakula kitakachoandaliwa na mpishi mkuu wa hotel hiyo.
Ziara ya balozi Auriol inaenda sambamba na juhudi nyingine za kutangaza kinywaji hicho hapa nchini, mojawapo ikiwa ni kampeni ya mabango ya ‘Flaunt Your Taste’ yaliyosambaa jiji zima pamoja na ukamilishaji wa chumba cha Hennessy kilicho katika Club 327, ambacho balozi Auriol atakizindua.
Balozi Auriol atakuwa na kikao maalumu pia na wapenzi wakubwa wa kinywaji hicho, na pia atawazawadia mialiko maalumu ya kuingia kwenye klabu ya wapenzi wa kinywaji hicho ya Afrika mashariki.
Pia atatoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu kutoka katika bar kubwa za jijini. Lengo kuu la mafunzo hayo yatakayofanyika katika hoteli ya Southern Sun na George & Dragon ni kuwapa wahudumu ujuzi utakaowawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa wateja wao wakati wakiburudika na kinywaji cha Hennessy kwenye bar au hotel wanazozipendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments: