Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi akiongea machache katika hafla ya kukabidhi vitabu kwa shule zipatazo 8 kupitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanayo kama ' AIRTEL SHULE YETU'. Hafla hiyo ilifanyika katika shule ya sekondari ya Yemeni iliyopo Keko jijini Dar es Salaam wiki iliyopita.
Mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi vitabu kwa shule za sekondari, kaimu afisa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya akizungumza machache kabla ya kukabidhi vitabu kwa shule zipatazo 8 kupitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanayo kama ' AIRTEL SHULE YETU'.
  Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi (Kulia) akimkabidhi vitabu mgeni rasmi, kaimu afisa mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kwanza kushoto) kwa niaba ya shule za sekondari zipatazo 8 kupitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ujulikanao kama ' AIRTEL SHULE YETU'. Walioshuhudia ni maofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kulia) akiwakabidhi vitabu Maofisa Elimu Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Kiduma Mgeni (Kushoto) na mwenzake kupitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ijulikanayo kama ' AIRTEL SHULE YETU'.
-->
Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kulia) akiwakabidhi vitabu wanafunzi wa shule ya sekondari ya Yemeni ambao walipokea kwa niaba ya wanafunzi wenzao. Pembeni anayeshuhudia ni Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi.
Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kulia) akimkabidhi vitabu mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Yemeni mwalimu Antipas Chale kupitia mradi wa upitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ujulikanao kama ' AIRTEL SHULE YETU'.
Kaimu Afisa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Michael Ole Mungaya (kushoto) akimkabidhi vitabu mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Alharamain ya Ilala, mwalimu Nuhu Mruma (kulia) kupitia mradi wa upitia mradi wa kugawa Vitabu kwa shule za sekondari ujulikanao kama ' AIRTEL SHULE YETU'. Katikati ni Meneja huduma kwa jamii wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania, Bi. Hawa Bayumi.
---
Mwishoni mwa wiki hii kampuni ya simu za mkononi ya airtel imetoa msaada wa vitabu kwa shule za secondary 8 za jijini Dar es Salaam vyenye thamani ya shilingi million 16 ambavyo kwa kiasi kikubwa vitasaidia kuondoa tatizo la upungufu wa vitabu kwa wanafunzi. shule ambazo zimebahatika kupata vitabu hivyo ni za jijini Dar es Salaam kutoka wilaya zote zikiwemo Seminary ya Al-Haramain,Whitelake,Mwambao, Hondogo B,Misitu,Yemen,Yeshua pamoja na Archbishop John Sepeku. akiongea wakati wa kukabidhi vitabu hivyo wakati hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika shule ya sekondari ya Yemen jijini Dar es Salaam –Temeke Kaimu Afisa Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Michael Ole Mugaya amesema kuwa shule nyingi zinakabiliwa na uhaba wa vitabu jambo linalopelekea walimu kuwa na wakati mgumu kipindi cha ufundishaji.
“ninafurahishwa sana na msaada huu ambao umezifikia  shule za mkoa wa Dar es salaam kwa mgawanyo sawa katika wilaya zote kwa kuwa kutokana na uhaba mkubwa wa vitabu pamoja na mahitaji mengine katika shule zetu huwapa walimu changamoto kubwa sana kufikia malengo yao, hivyo bado ninatoa wito kwa  taasisi nyingine binafsi na za serikali kuchangia katika elimu kama walivyofanya Airtel Tanzania” alieleza Michael Ole Mugaya.
Naye Meneja wa huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi amesema kuwa Airtel wameguswa na tatizo la ukosefu wa vitabu mashuleni ambao unapelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika mitahani ya mwisho.
“Vitabu hivi vipo katika mgawanyo sawia katika masomo mbalimbali kama jiografia, hisabati mpaka sayansi. Tunaamini kwamba kila mwanafunzi akiwa na kitabu chake ataweza kuwa makini darasani na baadaye kusaidia kuongeza ufaulu katika mitihani nchini” Alisema Bi. Hawa Bayumi.
Akizungumza kwa niaba ya waalimu wenzake wa shule zilizofaidika na mradi huo Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Yemen iliyopo Dar es Salaam, alisema kwamba wamefurashwa sana na mradi huo wa kijamii wa Airtel wa kugawa vitabu na kwamba huo ni msaada mkubwa sana katika shule zao.
“Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada wenu huu ambao lengo lake ni kufikia malengo ambayo sisi waalim tumejiwekea katika shule zetu ili kuboresha kiwango cha elimu kwa wanafunzi tunaowafundisha tunawaahidi kuvitunza ili vitumike kwa muda mrefu alimaliza kwa kusema Mkuu wa sekondari Yemen…”

Airtel kupitia mradi wake wa ‘Airtel shule yetu’ zaidi ya shule 93 za sekondari zinatarajia kunufaika na mradi wa unaolenga kugawa Vitabu na vifaa vingine vya kujifunzia kwa shule za sekondari nchini mwaka huu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: