Na Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Simon Mdugu mwenye
umri wa miaka (70) Mgogo, mkulima na mkazi wa Kisima cha Ndege Mundemu katika
wilaya ya Bahi amefariki Dunia baada ya kujeruhiwa na Ndoo Kichwani na katika
Taya na mteja wake aliyekuwa akichota maji katika kisima chake.
Akizungumzia tukio
hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Zelothe Stephen alisema tukio
hilo lililipotiwa Polisi mnamo tarehe Tarehe 07/ 10/2012 majira ya kumi na mbili
jioni (18:00 hrs) katika kituo cha
Polisi Wilaya ya Bahi.
Bw.
Zelothe alimtaja mteja huyo ambaye ni
mtuhumiwa katika tukio hilo kuwa ni Bi MAGRETH d/o JOSEPH, mwenywe umri
wa Miaka (44) Mgogo, Mkulima ambaye pia ni mkazi wa Kisima cha Ndege.
Kamanda
Zelothe Stephen alisema chanzo cha tukio
hilo ni Ugomvi ulitokea siku ya Jumamosi Tarehe 06/10/2012 Majira ya saa nne asubuhi
ambapo Marehemu alikuwa akimdai Bi MAGRETH d/o JOSEPH amlipe pesa Shilingi mia
mbili (Tsh 200/=) baada ya kuchota maji katika Kisima chake.
“Bw.
Simon Mdugu ambaye ni marehemu alimtaka Bi
Magreth Joseph aliyekuwa amejitwisha ndoo kichwani kumlipa pesa yake, mwanamke
huyo alikataa na mara ugomvi ukatokea ndipo akampiga na ndoo hiyo na kumjeruhi
Kichwani na katika Taya lake.” Alieleza Bw. Zelothe
Mkuu
huyo wa Polisi Mkoa wa Dodoma alisema baada ya mzee huyo kujeruhiwa alikwenda kupata matibabu
katika kituo cha afya cha Mdemu ambapo alitibiwa na kuruhusiwa kurudi nyumbani,
lakini Mnamo Tarehe 07/ 10/2012 majira ya 18:00 kamili jioni alifariki dunia
Kamanda
Zelothe Stephen alisema mtuhumiwa
amekamatwa na anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na
atafikishwa mahakamani mara moja kujibu tuhuma zinazomkabili.
Wakati
huo huo Gari namba T.624 BAD TOYOTA
CRESTA lililokuwa likiendeshwa na Jasiri Maligo, Miaka (44), Mbena, mkazi wa
Ipagara lilimgonga mtembea kwa miguu ambaye hakufahamika jina, mwanaume, umri
kati ya miaka 35-40 na kumsababishia
kifo.
Kamanda Zelothe alisema tukio
hilo lilitokea tarehe 07/10/2012 majira ya saa tatu usiku, katika eneo la
Chaduru kata ya Makole tarafa ya Mjini katika Manispaa ya Dodoma kwenye
barabara kuu ya DODOMA/MOROGORO.
Akizungmzia Chanzo cha
Ajali hiyo, alisema kuwa ni uzembe wa Dereva, aidha alisema Dereva wa gari hiyo
amekamatwa na atapelekwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments: