Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU)
Unapenda kuwakaribisha Watanzania
wote wanaoishi ujerumani, Katika Hafla ya WORLD MISSION SUNDAY. itakayofanyika Katika ukumbi Uliopo Hauptstr.
30, D-63814 Mainaschaff Jirani sana na Mji wa Aschaffenburg Siku ya
Jumapili Tarehe 28.10.2012,
Kuanzia saa 04:00 za Asubuhi. Ambapo Wasamaria wema na Wafadhili
wapatao zaidi ya 150 kutoka sehemu mbali mbali za ujerumani watakutana
na umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) Juu ya kuitakia mema Tanzania na
kuanzisha Harambee ya kuchangia maendeleo ya miradi mbali mbali
itakayosimamiwa na Umoja wa watanzania Ujerumani (UTU). Katika Hafla
hiyo Kuanzia saa 9 mchana watayarishaji wa Hafla hiyo ''World Mission Sunday''
itatoa nafasi kwa Umoja wa Watanzania Ujermani (UTU) Kuitambulisha
Tanzania Kwa wahisani hao , na kuelezea ni mradi gani unahitaji
ufadhili kupitia Umoja huu. Mmoja wa wageni rasmi walio alikuwa ni
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Ahmada Ngemera, Dr. Lippert na mkewe Kutoka Scheinfurt' Dr.
Lippert ni mtaalamu ambaye aliwahi kufanya kazi Tanzania. Hafla hii
inategemewa kuisha saa 12:00 za jioni, baada ya hapo watanzania watapata
muda wao wa kufanya mazungumzo na Mhe: Balozi wa Tanzania
Nchini ujerumani Bw. Ahmada Ngemera.
Umoja wa Watanzania Ujerumani UTU Umeramba Bingo kwa kupewa nafasi hii ya pekee Na WORLD MISSION SUNDAY Kuiwakilisha Jamii ya watanzania na kuwashawishi Wafadhili na wahisani nchini ujerumani ili waweze kuchangia Miradi mbali mbali ya Huduma za jamii nchni Tanzania ikiwemo sekta ya Elimu na Afya.
Tunawaomba Watanzania Wote na marafiki wa Tanzania wanaoishi Ujerumani na jirani mwa ujerumani, kuhudhuria kwa wingi katika Hafla hii muhimu kwa jamii ya watanzani kama wasemavyo wahenga ''CHEREKO CHEREKO NA MWENYE MWANA'' Kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com au unaweza kuwasiliana na Mwenyekiti Wa UTU moja kwa moja kupitia simu ya mkononi. 0173-4298997
Karibuni sana ! Umoja Ni Nguvu
Toa Maoni Yako:
0 comments: