Taasisi  Isiyokuwa  ya  Kiserikali  ya  RafikiElimu  FOUNDATION  kupitia  Mradi  wake   ELIMU  YA  UJASIRIAMALI  MIJINI &  VIJIJINI  “ EUMIVI-Project “  inapenda  kuwatangazia  vijana  wote  wa  kitanzania  wenye  umri  wa  kati  ya  miaka  kumi  na  tano (15) hadi Arobaini  na  Tano  (45) nafasi  za  kushiriki  katika  mafunzo  ya  ujasiriamali.
Mafunzo  yatakayo  tolewa  ni  pamoja  na :
i. Utengenezaji  na  Uzalishaji  wa  Bidhaa  za  aina mbalimbali  kama  vile  :
a.  sabuni  za  aina  zote
b. batiki
c.  Chaki  za  aina  zote.
d. Mishumaa.
e. Usindikaji   wa  vyakula, vinywaji& matunda
f. Uokaji  wa  mikate,
g.    utengenezaji  wa  bidhaa  za  ngozi  kama  vile  mikanda  na  viatu  kwa  kutumia  ngozi  za  wanyama  zilizo  sindikwa.
h.    Utengenezaji  wa  viungo  vya  vyakula  vya  binadamu  kama  vile  Chilli  Sauce, Tomato Sauce, Mango Picco , Peanut Butter nakadhalika.
i.       Utengenezaji  wa   mkaa  kwa  kutumia  makaratasi.
j.       Utengenezaji  wa  kiwi.
k.    Utengenezaji  Wa  Vyakula   Vya  Mifugo  kama  vile  kuku na  n’gombe.
l.       Mbinu  Za  Ufuaji  Bora.
m. Mbinu  za  kilimo  Bora.
ii. Elimu  Ya  Ujasiriamali.
iii. Elimu  Ya   Sheria  Za  Biashara.
iv. Elimu  Ya  Usimamizi  na  Uongozi  Wa  Biashara.
v. Ubunifu, Uendeshaji  na  Usimamizi  Wa  Miradi
vi. Uandishi  Wa  Miradi Mbalimbali.
vii. Elimu  Ya  Uwekaji  na Ukopaji  Fedha  .
viii. Elimu  Ya  Uendeshaji  wa  Vikundi  Vidogo  Vidogo  Vya  Kuweka  na  kukopa   Fedha.
ix. Elimu  Ya  Utengenezaji  na  Utafuta  wa  Masoko.

ADA  YA  USAJILI :  Ada  ya  kujisajili  katika  mradi  huu  ni  BURE.
ADA  YA  MAFUNZO :  Ada  ya  kushiriki  katika  mafunzo  haya  ni  BURE.
MWISHO   WA  KUJIANDIKISHA  : Tarehe  25  OKTOBA  2012.
KUANZA   KWA  MAFUNZO    :   Tarehe    01  NOVEMBA  2012.
KUZINDULIWA  KWA  MRADI  :  Tarehe  23  OKTOBA  2012.

NAMNA  YA  KUJIANDIKISHA :  Fika  katika  ofisi  zetu  zilizopo  katika  eneo la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA  TAKWIMU.
Panda  gari  za  UBUNGO  -  CHANGANYIKENI,  kisha   shuka  kituo  kinaitwa  TAKWIMU. Ukifika  TAKWIMU fuata  barabara  ya  lami  hatua  ishirini (20) kisha  tazama  upande  wako  wa  kulia  utaona  bango  la  ofisi  yetu limeandikwa RAFIKIELIMU  FOUNDATION.

Kwa    maelezo  zaidi  wasiliana  nasi  kwa  simu
               0763976548 AU 0782405936.

Kwa  taarifa  zaidi  kuhusu Mradi Huu, tembelea  blogu  yetu :  www.rafikielimu.blogspot.com

WAHI  NAFASI YAKO MAPEMA KWANI  NAFASI  ZILIZOPO  NI  CHACHE.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: