Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.

Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la KwelaMh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.



Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw. Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na kwamba wanatarajiwa kufikishwa wakati wowote mahakamani.
Baadhi ya matrekta yaliyoteketezwa kama yanavyoonekana
Moja ya makambi yaliyoteketea kwa kuunguzwa na moto wakati wananchi hao walipovamia mashamba hayo na kuchoma moto zana za kilimo katika shamba hilo. PICHA NA HABARI: http://gospelvisiontz.blogspot.com/
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: