Dereva wa Bodaboda na abiria wake, ambao hawakuweza kufahamika majina yao kwa haraka, wakiwa wamelazwa pembeni mwa barabara ya Bagamoyo eneo la Makongo, baada ya kugongwa na gari aina ya Starlet yenye namba za usajiri T 838 BKB, wakati wakiwa katika Pikipiki yao yenye namba za usajiri T 491 BFY, na kufariki dunia papo hapo. Ajali hiyo ilitokea jana asubuhi, Pichani ni raia akijaribu kutambua mwili wa marehemu katika ajali hiyo. Picha na www.sufianimafoto.blogspot.com
Kiukweli yapo mambo mengi ambayo yanatokea ila hili lilinisikitisha sana kwa vile ajali hii niliishuhudia mwenyewe nilipokuwa naenda Mbezi beach muda wa saa 12:12asbuhi niliogopa kupiga picha kwa vile ilikuwa imetokea eneo la Jeshi la Polisi. Japo mimi ni mwandishi wa Habari ninayetambulika na kutambuliwa na Serikali lakini ilibidi niwe mpole tu nipite niendelee na mambo yangu. Natambua wote mnajua eneo la Jeshi huwa haziruhusiwi kupiga picha. Ni mimi Cathbert Angelo Kajuna mmiliki wa Kajunason Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: