Mwananafunzi wa shule ya Sinza Maalum akiimba wimbo wa mwanamuzi Ambwene Yesaya (AY) walipotembelewa na mwanamuzi huyo mwishoni mwa wiki hii wakiongozana na wafanyakazi wa Airtel, kushoto ni meneja mahusiano wa jamii wa Airtel Hawa Bayumi, watatu kutoka kulia Ambwene Yessaya (AY) akifwatiwa na Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki.
Balozi wa Airtel Ambwene Yesaya (AY) wakiimba kwa pamoja na
mwanafunzi wa shule ya Sinza Maalum (Kushoto) mwishoni mwa wiki hii
walipotembelewa na mwanamuzi huyu aliyeongozana na wafanyakazi wa
Airtel kama mwendelezo wao wa kusaidia jamii kwa watoto wenye
mahitaji maalum kupitia mradi wao wakishirikiana na Bamvita wa
kuchangia Elimu.
Wafanyakazi wa Airtel wakiwa na balozi wao Ambwene Yesaya katika
picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya sinza Maalum iliyopo jijini
Dar Es Salaam walipotembelea shule hiyo mwishoni mwa wiki hii kama
mwendelezo wao wa kusaidia jamii kwa watoto wenye mahitaji maalum
kupitia mradi wao wa kuchangia Elimu kwa kushirikiana na BAMVITA.
---
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia kitengo chake cha
huduma kwa jamii imeanza mchakato wa kutembelea baadhi ya shule
zitakazonufaika na mradi maalum wa kuwasaidia watoto wenye mahitaji
maalum ili kujionea changamoto zinazowakabili pamoja na kuwahimiza
watanzania kuweza kuchangia mradi huo unaoendeshwa kwa ushirikiano na
Baraza la maendeleo ya vitabu Tanzania (BAMVITA).
Afisa mawasiliano na matukio wa Airtel Bi Dangio Kaniki amesema
kampuni hiyo ikiwa na Balozi wake msanii Maarufu AY itatembelea shule
zote zilizopo Dar es Salaam pamoja na mikoani na kubaiunisha matatizo
wanaoyokumbana nayo ili kuona namna ya kuwasaidia.
Amesema shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum zinahitaji
vitendea kazi vingi ili kuwafanya wanafunzi hao kuweza kupatiwa elimu
inayostahili.
“Shule hizi zinamahitaji mengi sana, Airtel tumeona ni vyema
kumtumia pia Balozi wetu huyu msanii maarufu nchini A Y kuendea
kuwafikishia jamiii ujumbe waendelee kuchangia katika mradi huu wenye
lengo la kuendeleza jamii” alisema Bi DANGIO KANIKI Afisa
mawasiliano na matukio wa Airtel.
Akizungumza mara baada ya kutembelea shule ya msingi Sinza Maalum
Balozi wa Airtel AMBWENE YESAYA (A.Y) amesema kukamilika kwa mradi
huo kutasaidia kuongeza kiwango cha elimu kwa watoto wenye mahitaji
maalum.
“Watoto hawa wenye uhitaji maalum nimejionea mwenyewe kuwa
wakiwezeshwa wanaweza, ndio maana naona ni vyema zaidi kushirikiana
na Airtel pamoja na jamii kwa ujumla kuhakikisha tunawachangia vijana
wetu hawa nao waweze kuendeleza hata vipaji vyao pamoja na elimu yao.
Ninaomba kuwakubusha watanzania kuchangia katika kuwapatia vijana
hawa vifaa mbalimbali ambavyo ni changamoto kwao, unaweza kuchangia
kwa kupitia Airtel Money ambapo unaandika jina la fumbo VITABU na
utatuma kiasi chochote au kwa kutuma SMS yenye neno VITABU
kwenda namba 15626 na atakuwa amechangia shilingi 200 tu.
Watanzania naomba tusaidiane katika elimu kwa kuwa tuanaamini
Tanzania itajengwa na sisi wenyewe. Alimalizia kusema AMBWENE YESAYA
---Balozi wa Airtel.
Wakati wa ziara hio mwuishoni mwa wiki hii Mwalimu Mkuu wa shule
ya Sinza Maalum, SIMON Milobo alibainisha kuwa shule hiyo inakabiliwa
na changamoto mbali mbali ikiwemo uhaba wa vifaa vya kufundishia
pamoja na mafuta ya kuendeshea gari la wanafunzi.
Kampeni ya Airtel kwa kushirikiana na Bamvita
itaendeshwa kwa muda wa miezi mitatu , na Watanzania wataweza
kuchangia kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na
kwakufanya hivyo kila SMS utakayotuma utakuwa umechangia shilingi 200
itakayoingizwa katika mradi huu”
Toa Maoni Yako:
0 comments: