Na Mwanshi wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Jeshi la
Polisi zanzibar limetangaza kuzifunga baadhi ya barabara za mji wa
Zanzibar ili kuwawezesha wananchi wakiwemo watoto wadogo kusherehekea
siku kuu ya Eddi el Haji kwa usalama na amani.
Afisa
Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina,
amezitaja baadhi ya barabara zitakazofungwa kwa muda wa siku nne kuanzia
Ijumaa wiki hii hadi Jumatatu wiki ijayo kuwa ni ile inayotoka Mnazi
Mmoja hadi Viwanja vya michezo vya Maisala, barabara ya kutoka Ofisi ya
Baraza la Wawakilishi la Zamani kuelekea Viwanja vya Maisala na Barabara
ya ya kutoka Ukumbi wa CCM kuelekea Mnazi Mmoja.
inspekta
Mhina, amesma kuwa barabar hizo zitafungwa kuanzia majira ya saa 9.00
arasili hadi saa 4.30 usiku kwa kila siku muda ambao watu wengi watakuwa
wamesharejea majumbani kwao baada ya kusherehekea siku hiyo.
Awali
akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mjini Zanzibar, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mjini Magharibi Ungauja ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa
sherehe hizo zitaadhimishwa kwa muda wa siku nne mfululizo zitaanza
Ijumaa ya Oktoba 26 hadi Jumatatu ya Oktoba 29 2012.
Katika
hatua nyingine Kamanda Aziiz amesema Jeshi la Polisi mkoani humo
litaweka vituo vidogo vya Polisi katika maeneo yote ya viwanja vikubwa
vitakavyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu kwa lengo la kuwahakikishia
wananchi ulinzi wa usalama wao pamoja na mali kwa wakati wote wa
sherehe hiyo.
Kamanda
huyuo amevitaja viwanja vitakavyokuwa na mikusanyiko mikubwa kwa ajili
ya sherehe hizo za Eddi El Haji kuwa ni Mnazi Mmoja, uwanja wa
Demoklasia, Jamhuri Garden, Forodhan Park, Kiembe Samaki, Nyarugusu,
Maungani na Bububu Meli nne.
Kamanda Aziz amesema Kiwanja cha michezo cha Kariakoo mjini Zanzibar kwa mara nyingi hakitaweza kutumika kutokana na kuharibika.
Amewataka
waqzazi na walezi kutowapa vijana wao makundi makubwa ya watoto wadogo
ili kuepuka kupoteana katika viwanja hivyo ambavyo mara nyingi vinakuwa
na umati mkubwa wa watu.
Amewakumbusha
wazazi na walezi hao pia kutowaruhusu watoto wao kwenda karika fukwe za
bahari kuogelea pasipo uwangalizi wa watu wazima kwani amesema kuwa
uzoefu unaonyesha kuwa watoto huzama na kufa maji baharini pasipokuwa na
uwangalizi katika nyakati za siku kuu kama hizi.
Hata
hivyo Kamanda Aziz amewataka wazazi kuwaelimisha watoto wao kuwa
wanapobaini kupotezana na ndugu na jamaa zao wafike katika vituo hivyo
vidogo vya Polisi na yeyote atakayepotelewa aweze kufika hapo kwa
utambuzi na kumpata mtoto wake.
Amewakumbusha
wananchi kutoziacha nyumba na sehemu zao za biashara pasipo na
uwangalizi wa kutosha wanapotoka kwenda katika viwanja vya burudani ili
kuepuka kuwapa wezi fursa ya kupora mali zao.
Kwa
upande wa madereva kamanda aziz amewataka madereva wote kuendesha vyombo
vyao kwa mwendo wa kadri na kuepuka kuvunja sheria, taratibu na kanuni
za usalama barabarani na kwamba kwa yeyote atakayekaigi agizo hilo hatua
kazi zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kukamatwa na
kufikishwa mahakamani.
Visiwani
Zanzibar sherehe za Eddi El Fitri na Iddi El haji ndizo sherehe kuwa
kupita zote za kiserikali na husherehekewa kwa muda wa siku nne
mfululizo katika viwanja mbalimbali ingawa utaratibu huo wa kusherehekea
hauingiliani na na ule uliopo kwenye kalenda ya Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: