MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na aliyekuwa bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni Jumamosi mwaka huu kuoneshana umwamba.
Cheka na Nyilawila walitwangana mbambanmo wao uliofanyika morogoro ata hivyo ulizua utata baada ya mpambano wao kugubikwa na alama za mshangao ambalo cheka aliibuka na ushindi wa point  mashabiki kuhisika wa mabondia hao wanaogopana na kutafutana kwa mda mrefu watapoza kiu yao kwa mpambano huo jumamosi ya kesho.

Akizungumza Dar es Salaam jana, promota wa pambano hilo Oswald Mlay alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa PTA Sabasaba.
 
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 12 uzito wa kg 72 ambapo leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano uho utakaoamua nani zaidi

Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: