Mwili wa marehemu Beatha 12 aliyepotea takribani siku kumi  wakutwa kichakani ukiwa umechunwa ngozi , kukatwa sehemu ya ulimi na kuondolewa sehemu za siri, tukio hili limetokea kijiji cha Mayondwe Muhutwe jimbo la Muleba Kaskazini.
  Tukio hili limepelekea wananchi wa Kijiji cha Muhutwe kushambulia kituo cha polisi na kumshambulia mzee mmoja mkazi wa Kijiji cha Ntungamo- Izigo  aliyekua amekamatwa kwa kuhusishwa na sakata hili la uchunaji wa ngozi.
Tunaendelea kuwataka radhi wadau wasomaji  kuhusiana na matumizi ya picha hizi za kutishakutisha.
 Kushoto ni daktari aliyedhibisha hali hii baada ya ukaguzi  akisaidiana na askari polisi kubeba mwili wa marehemu Beatha.
Mwili ukiwa tayari umehifadhiwa katika sanduku na matukio kama haya yamekua yakijirudia  maeneo ya Muhutwe jimbo la Muleba Kaskazini, hadi wananchi kuchukua hatua mikononi na kushambulia kituo cha polisi ikiwa ni tukio jingine kwa madai watuhumiwa wanaokamatwa wamekuwa wanaruhusiwa kirahisi na polisi wa  eneo hilo... Shukrani kwa Mc Baraka wa BukobaWadau Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: