Wa
kwanza ni injinia wa Airtel mkoani Iringa bw Joshua Kadege akitoa ufafafanuzi kwa mwenyekiti wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo
la Isimani bw Anderson Mpululu jinsi mtambo wa mawasiliano uliowekwa na
Airtel kijiji hapo unavyofanya kazi ili kurahisisha mawasiliano katika
kijiji hicho.Airtel imeanza kufunga mitambo ya mawasiliano itakayotumia
nguvu za Nishati ya jua (solar) ili kufikisha mawasiliano
katika maeneo ya vijijini, kati ni meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania bw
Jackson Mmbando wakati wa hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika kijijini
Kimande nje ya mji wa Iringa jana.
Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na bw Beda Kinunda Meneja wa Mauzo wa airtel Mkoani Iringa wakiwa nje ya Mnara wa Airtel unaotumia nguvu ya Nishati ya jua (solar) wakizungumza na Mwenyekiti wa
kijiji cha Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu (shoto) mara
baada ya Airtel kuzindua rasmi mnara wa mawasiliano unaotumia nguvu za
Solar katika kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani,
Airtel imezindua mnara huo unaotumia nishati ya jua kwa lengo la
kufikisha mawasiliano katika maeneo ya vijiji ambapo bado hakujafikiwa
na umeme wa taifa.
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa kijiji
cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson Mpululu
kuhakikisha wanaweka ulinzi shirikishi kulinda mtambo mpya wa
mawasiliano unaotumia nishati ya jua uliowekwa na Airtel ili kufikisha huduma bora ya mawasiliano kijijini hapo, wakwanza kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel Nyanda
za juu kusini Bw, Beda Kinunda na kushoto ni Injinia wa Airtel mkoani
Iringa bw Joshua Kadege. Hafla ya uzinduzi ilifanyika kijijini Kimande
nje ya mji wa Iringa jana.
Kulia
ni Injinia wa airtel mkoani Iringa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti
wa kijiji cha Kimande tarafa ya Pawaga-Jimbo la Isimani bw Anderson
Mpululu anaedadisi ili kupata ufafanuzi wa jinsi mnara wa Airtel
unaotumia Nishati ya jua (solar) unavyofanya kazi mara baada ya Airtel
kuzindua mnara huo kijijini hapo jana
Toa Maoni Yako:
0 comments: