Utangulizi
Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa
umma, kuhusu tetesi zilizokuwa zimeenea hapa
nchini kutoka kwenye vyombo mbali
mbali vya habari kuhusu
kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola, wilayani Karagwe mkoa
wa Kagera.
Mnamo
tarehe 3 Agosti 2012, Wizara ya Afya na Ustawi Wa
Jamii ilipokea taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa
wilaya ya Karagwe ya kuwepo kwa mgonjwa aliyekuwa
anahisiwa kuwa na dalili za ugonjwa
wa Ebola, katika hospitali ya Wilaya ya
Nyakahanga. Aidha, taarifa hiyo ilibainisha kuwa mgonjwa
huyo alikuwa ni mtoto wa
kiume mwenye umri wa miaka (6)
kutoka katika kijiji cha Nyakatundu wilayani Karagwe.
Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali, kulegea, kutokwa damu
puani, kutapika damu, na kukojoa damu.Maelezo kutoka
kwa mama mzazi zilieleza kuwa mtoto
huyu alianza kuugua kuanzia tarehe 30 Agosti
2012, ambapo alipatiwa dawa ya Septrin baada ya
hospitali binafsi kuonyesha kuwa ana ugonjwa wa “Typhoid”.
Uchunguzi
wa awali katika hospitali ya Nyakahanga ulionyesha kuwa mtoto
huyu alikuwa anasumbuliwa na uambukizo kwenye haja ndogo (Urinary
Tract Infection). Vile vile alifanyiwa
uchunguzi wa kimaabara na Vipimo vya malaria,
Hepatitis na Typhoid havikuonyesha kuwepo kwa magonjwa haya.
Hospitali inaendelea kumpatia matibabu mtoto huyu na imewaweka
mgonjwa na mama yake anayemtunza kwenye chumba maalum (Isolatiom
room) kwa ajili ya uangalizi zaidi.
Aidha
mnamo tarehe 4 Agosti 2012, timu za wataalamu
kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Kagera
imeweza kufika na kumfanyia uchunguzi wa kina
pamoja na kuchukua sampuli za damu kwa ajili ya uchunguzi
zaidi katika maabara ya Taifa ya
uchunguzi wa magonjwa na Maabara za nje ya nchi,
ili kubaini kama ameathirika na ugonjwa wa Ebola. Timu
hiyo ya wataalamu imetoa taarifa kuwa hali ya
mgonjwa huyu kwa sasa
imeimarika ikiwa pamoja na
kutokuwa
na homa,
kutapika
na
kukojoa damu kumekoma
pia,
uchunguzi uliofanywa kwa mama wa mtoto umeonyesha
kuwa
hana
dalili
zozote
za
ugonjwa wa Ebola.Vile
vile hakuna taarifa ya mtu mwingine yeyote kwenye familia
hiyo
au
kwenye maeneo ya kijiji hicho au cha jirani kuwa na dalili za ugonjwa
huo.
Kufuatia
taarifa hii, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na
Mkoa wa Kagera imechukua hatua zifuatazo;
1.
Imepeleka timu
ya
wataalamu mbali mbali kutoka Wizarani
na mkoa
kwa lengo la kwenda kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu
kuwepo
kwa ugonjwa huo.
2.
Imetoa elimu
ya Afya
kuhusu njia
za kuzuia kuenea
ugonjwa
wa Ebola pamoja na dalili za ugonjwa huu,
kwa
wananchi
na watumishi
wa afya katika hospitali ya Nyakahanga
4
Kupeleka vifaa kinga katika
hospitali
ya Nyakahanga
pamoja
na maeneo ya mipakani.
5. Kutoa
matangazo kwa jamii kwa kutumia vipaaza sauti na
kupitia
radioni (Radio Karagwe) kuhusu ugonjwa huu
6.
Aidha, vipeperushi pia vimetolewa.
Hitimisho
Wizara
inapenda kuufahamisha umma kuwa mpaka sasa hakuna
mgonjwa yeyote aliyethibitishwa
kuwa na ugonjwa wa Ebola hapa
nchini.Aidha, Wizara ya Afya imejiaanda
kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huu iwapo utatokea hapa nchini.
Kwa
sasa timu za wataalum
zipo katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro na
Arusha, kutoa elimu juu ya ugonjwa
huu kwa wataalamu na kwa wananchi na
vilevile kufuatilia ugonjwa huu sehemu za mipakani.
Wizara
inaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwenye kituo
chochote cha kutolea huduma za afya,
mara wanapoona dalili za ugonjwa huu.
Imetolewa
na:
kitengo
cha Mawasiliano
Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii
Tarehe
6 Agosti, 2012
Toa Maoni Yako:
0 comments: