Mwalimu Daniel Urioh. |
Ninaomba
WIZARA YA ELIMU iwe makini na wawekezaji katika secta ya elimu, hasa
kwenye shule ambazo zinatoa msaada kwa watoto wakitanzania ambao
familia zao hazina uwezo wa kifedha, kwa mfano ninaomba mmiliki wa
shule ya St Jude apate muda wa kusikiliza kilio cha wafanyakazi wake
wakitanzania kwani kimsingi wamekuwa wakiteswa, kukandamizwa na
kupuuzwa wanapodai haki na maslahi bora kazini kwao.
Shule
hii utumia picha za wafanyakazi kuzalisha kiasi kikubwa cha fedha
kuendesha shule, kwa wafanyakazi na wanafunzi hupigwa picha mara kwa
mara na kulazimishwa kuleta picha za familia zao kila mwaka bila
shule kuweka wazi kwa mfanyakazi kuwa anawafadhili wangapi,
wafadhili huchangia kiasi gani cha fedha, kukatazwa kuwasiliana
na mfadhili, kuruhusiwa kuhoji lolote kuhusu pato na matumizi ya
uzalishwaji wa fedha kupitia wewe na familia yako? Hata hivyo picha
za familia zinazalisha fedha kwaajili ya uendeshaji wa shule ilihali
familia haifaidiki kwa uuzaji huo wa sura zao ughaibuni?
Kinachosikitisha zidi ni pale mfanyakazi anapoachishwa ,shule
inaendelea kitumia picha za wafanya kazi na familia zao kuzalisha
fedha nyingi za kigeni bila ridhaa wala fedha hizo kuwafaidisha wenye
picha, na kutojali kuwa kitendo hicho kinyume na sheria.
Pia
picha hizo zimekuwa mara kadhaa zikidhalilisha utu na uhuru wa
muafrika, kwani sura za watanzania zimekuwa bidhaa ya kuzalisha fedha
zisizojulikana ni kiasi gani na kwa faida ya nani? tena ulazimisha
vitendo visivyo halisi na maisha yetu mfano unalazimishwa kucheka
ukichukuliwa picha ilihali mapato uzalishayo hujui na ukikataa
kutekeleza unatishiwa kufukuzwa kazi, wanafunzi ushikishwa zawadi
zisikuwa zao na kupigwa picha na uzalisha kiasi cha fedha bila ridhaa
wafunzi wanapohoji hupewa adhabu au kutishiwa kufukuzwa.
Kama
hiyo aitoshi shule hii imekuwa mara kadhaa ikipuuza sheria za nchi
bila sababu za msingi mfano wamekuwa wakiajiri familia za ughaibuni
kinyume na sheria za nchi mfano wanaajiri baba, mama na mtoto wa
familia moja tena kwenye nafasi za juu na kutoweka wazi taaluma zao
wakiwaaminisha kuwa ukiwa mzungu basi we msomi wa kila kitu, kinyume
na sheria ya ajira nchini, pia shule imekuwa mara kadhaa haieshimu
sikukuu za kitaifa bila sababu za lazima na kutojali wala kuthamini
mchango wa waasisi na wazalendo waliopoteza maisha kujenga utaifa,
amani na umoja wa Tanzania, cha kushangaza shule ujiamulia siku za
mapumziko ya wafanyakazi na wanafunzi watakavyo wao, huwa najiuliza
hivi shida inaweza tulazimisha kufuata sheria za wawekezaji na
kupuuza sheria za nchi yetu Tanzania?
Linalosikitisha
zaidi shule hii imekuwa hodari wa kupiga vita ya matumizi ya lugha ya
kishwahili kwa wanafunzi na wafanyakazi hata kudiriki kuwaadhibu kwa
kuwarudisha wanafunzi nyumbani kwa kosa la kuzunguza kishwahili, hata
kufika mbali zaidi na kufukuza mwalimu mwenye shahada ya ualimu kwa
kosa ni kuzungumza kishwahili na wanafunzi, huu ni uvunjaji wa sheria
za nchi usiovumilika.
Hata
hivyo nataka wao wajue kuwa lugha ya taifa Kiswahili imekuwa mhimili
mkubwa wa kujenga umoja na amani. Kiasi cha kuwa wekeza kupata
mafanikio, kama awa amini wakajaribu kuwekeza Somalia na kuwasaidie
watoto wa Somalia wenye shida kubwa ya elimu, ilo linge ondoa jeuri
yao ya kupuuza sheria za Tanzania.
Kitendo
cha shule hii kuwatumia watanzania kama bidhaa na utaratibu wao wa
fukuza fukuza waliyonayo hasa kwa watanzania. Shule hii
huwatumia viongozi wazalendo kuwanyanyasa wenzao na kusaidia shule
kuendelea na dharau na kupuuza sheria za nchi zenye maslahi kwa
wazalendo, wale wote watakaonyesha uzalendo kama mimi wakuonyesha
kukerwa na kuchukua hatua ya kuhoji na kutetea sheria za nchi na
watanzania dhidi ya upuuzwaji wa uzalendo, haki, utu, lugha ya taifa,
maslahi ya kiwango cha utumikishwaji, niliishia kufukuzwa kwa kosa la
kuongea kishahili na wanafunzi.
Ushauri
wangu kwa wizara ya elimu.
Kwanza
kupandisha mshahara na mazingira ya kazi serikalini ilikuvutia
waalimu wote toka shule binafsi kwani wangi wamechoshwa ni manyanyaso
ya waajiri.
Pili
kufanya ukagua si wa taaluma tu bali pia mfumo wa uajiri na maslahi
ya watanzania waajiriwa kwenye shule zinazomilikiwa binafsi kwa
misaada ya watu toka ughaibuni.
Tatu
iwe na utaratibu wa ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya shule
zinazopata fedha toka kwa wafadhili kwani shida za watanzania
zimekuwa zikinufaisha wachache na kutengeneza ajira ya watu wasiona
sifa za kufanya kazi ughaibuni na kuja kufanya kazi ambazo wazalendo
wanaweza kuzifanya.
Nne
kusisitiza hasa shule binafsi nchini kuthamini lugha ya kishwahili,
kuheshimu sheria za ajira, kuheshimu sikukuu za kitaifa na kuheshimu,
kulinda tamaduni na vipaji vya watanzania kwa manufaa ya
Tanzania.
Ni
kweli tar 15/06/2012 nimefukuzwa kazi ya kufundisha (ualimu)
St-Jude-Arusha kwa kosa la kuzungumza Kiswahili.
Uzalendo
gharama nimeamua kujitoa kwa kutetea nchi yangu Tanzania.
Mwalimu
Daniel Urioh. Kwa undani zaidi piga :+255 755 379 737
Kamanda kajunason inasikitisha sana nikiwa kama mwana blog stori hii tutawafikishia wana diaspora ili kuijadili zaidi, ila wakati naisoma nilitokwa na machozi na kujiuliza Tanzania tunakoelekea ni wapi...? Pole sana Mwalim ila tupo pamoja na wewe kuufikisha ujumbe huu kwa Wtanzania wote walio ughaibuni!
ReplyDeleteNakushukuru sana mchangiaji kwa kuwakaripia hawa ndugu zetu wanaofanya kazi huko Marekani kwa kutokutambua uzawa kwanza.
ReplyDeleteKwanza kabisa kama ningekuwa mwanasiasa ningemuunga mkono mchungaji Christopher Mtikila na sera zake za uzawa. Nasema hivyo kwasababu wakati Mheshimiwa Mtikila anazungumzia Uzawa ni watanzania wachache sana waliomwelewa.
Lakini ukweli wa neno hilo umetafriwa na msemaji aliyepita alipotoa mfano wa mwanafunzi wa udaktari anapokwenda kuchukua mafunzo katika nchi zinazotumia lugha tofauti na kiingereza.
Amegusia uzawa kwa nchi hizo kutaka kujifunza lugha ya kwao kwanza. Mimi naenda mbali zaidi katika nchi kama marekani kama wewe ni daktari , mhasibu , au mtaalamu yoyote na umetoka Tanzania na vyeti vyako/ nondo kama wanavyoziita hakuna mahali popote utapata ajira kwa vyeti hivyo ni lazima uingie kwenye vyuo vyao
Tumeona swala la ajira kwa wawekezaji kama alivyosema Urio kuwa familia nzima ipo kwenye menejiment bila kujali elimu walio nayo na serikali inakaa kama haioni. Angekuwepo Mtikila kwanza wakurugenzi wangekuwa wazawa wenye vyeti vinavyolingana na stahili ya uwekezaji huo.
Kama alivosema urio watu wenye rangi nyeusi tumekuwa tunawaogopa watu wenye rangi nyeupe siyo tu hapo Tanzania hata huku ughaibuni wanafanya kama wao ni mungu watu kwa rangi nyeusi
Pamoja na kuwa ni sekta binafsi ni lazima kuheshimu sheria za nchi zilizopo , na kama alivyosema mheshimiwa Raisi alivyokuwa anazungumzia raslimali za nchi hususan gesi ni wakati umefika sheria zitungwe kwa maslahi ya watanzania na sio wageni ili watanzania kunufaika na raslimali zetu katika secta zote, ziwe binafsi au serekalini
Msemaji aliyepita amezungumzia mshahara duni ni kweli kwani hizo dola chache wanazolipa hazikidhi zaidi ya kulipa kodi ya chumba kama unataka maisha mazuzi zaidi ufanye kazi mbili hadi tatu na hatimaye kukaribisha kifo mapema kwa kukosa usingizi
Serikali ikisimamia vizuri sekta binafsi hatimaye watanzania tulioko ughaibuni tutarudi nyumbani kuja kufanya kazi bega kwa bega na wawekezaji ili kujenga nchi yetu.
Nchi hizi za ughaibuni zinapendeza kwa vile wameiba sana raslimali zetu ni wakati sasa kupinga kwa nguvu zote mipango mibovu ya uwekezaji wao kwani tumeshagundua janja yao
Kwa kusimamia haki ni sharti mwalimu Uriyo arudishwe kazini na hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya wanahusika kwa aliyo yataja.
Mungu ibariki Tanzania dumisha amani na upendo kwa watu wote wenyeji na wageni
Nakushukuru sana mchangiaji kwa kuwakaripia hawa ndugu zetu wanaofanya kazi huko Marekani kwa kutokutambua uzawa kwanza.