Naibu mwenyekiti na afisa mkuu wa shirika la Standard Group Paul Melly amejiuzulu. Akitoa tangazo hili, Mwenyekiti wa bodi ya usimamizi ya standard group Robin Sewell amemshukuru Melly kwa mchango wake mkubwa katika kuikuza kampuni ya standard group. melly alijiunga na kampuni ya standard group mnamo desemba mwaka wa 2004 kama naibu mwenyekiti na mshauri wa mikakati. Baadaye alipandishwa ngazi na kuwa afisa mkuu mtendaji. Kwenye tangazo lake, sewell amesema bodi ya standard itaanza mikakati ya kumtafuta mtu atakayechukua nafasi ya melly anayetarajiwa kuondoka katika kipindi cha miezi sita ijaayo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: