Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake.
Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) akiwa mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation).
Mwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguli.
Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni.
Mama Mzazi wa Agnes akilia kwa uchungu baada ya kuona mwili wa Mwanae.
Aliyevaa Koti jeusi ndio baba mzazi wa Agnes Bwana Bernard King'unza.
Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake.
Baba Padre wa Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King'unza.
Hawa ni baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM.
...
Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.
Marehemu Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.
Toa Maoni Yako:
0 comments: