Na Mwandishi Wetu
 
MFALME wa nyimbo za asili nchini, Costa Siboka, anatarajia kuzindua albam yake ya ‘Nderule’ kwenye  msimu wa sherehe za Nanenane mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa udhamini wa kinywaji cha Konyagi.

Akizungumza na  Kajunason Blog jijini Dar es Salaam,  Siboka alisema kua  amejiandaa vya kutosha kwa udhamini huo mkubwa wa kapuni ya Tanzania Distilleries Limited watengenezaji wa Konyagi,  ambapo aliwashukuru na kuwaadi mashabiki wake kujitokeza kwa wingi Mkoani Shinyanga,  Agost 8, siku ya  Nanenane na baada ya hapo ataendelea mikoa mingine ya Kanda hiyo ya Ziwa.

“Bendi yangu  imejiandaa vya kutosha  kwa uwezeshwaji wa bia ya Konyagi, tutapiga shoo sambamba na uzinduzi wetu  wa Albam ya pili ya  ‘Nderule’ hivyo  tunaomba kujitokeza kwa wingi wakazi wa Shinyanga hiyo siku ya Nanenane” alisema Siboka.

Siboka  aliongeza  kua, mbali na  uzinduzi wa Albamu hiyo  ya pili, pia bendi yake itafanya kweli kwa mashaibiki wake wake kwa kuonesha vitu vipya na kusuuza roho zao kutoka kwa wanenguaji wake wakiwemo wa zamani na wapya, ambao ni pamoja na Halima Ndembendembe, Fadhira Mitikisiko, Salama Kadogoo na Queen Mwanasesere, ambao  wote walipata  mafunzo kutoka Chuo cha Sanaa Bagamoyo.

Pia alizitaja nyimbo  ziizo kwenye albam yake hiyo  yenye nyimbo sita, kua ni pamoja na ‘Butereakaila’, Busoma basi’, ‘Omwana  kalikwela’  na zingine nyingi.
Aidha, alisema mashabiki wake kwenye ziara hiyo watabahatika na kuzisikia na nyimbo zake zinazotamba za albam yake ya kwanza ya ‘Niwewange’ ambapo nazo atazipiga kwa mashabiki wake, aliwataja wadhamini wengine kua ni Balimi Extra, Zizou fashion,Sisi entertainment, CXC Africa, Precision air na wengine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: