Meli ya Mv Skagit iliyokuwa safarini kutoka Dar kuelekea Zanzibar imezama majira ya saa nane mchane hivi leo katika maeneo Pungume na Chumbe baada ya kukumbwa na upepo mkali.
Meli hiyo inayosadikiwa kuwa na abiria 250 inasemekana imepindukia upande mmoja na huku abiria wengi wakiweza kuokolewa kutokana na jitihada mbali mbali kupitia vile vile msaada wa boti za Mv Kilimanjaro, Tug ya Bandari na vyombo vyengine.
Mpaka tunandika taarifa hizi ni maiti tatu zilikwishapatikana na kiasi cha abiria 150 wameokolewa na waliojeruhiwa wanatibiwa katika Hospitali ya Mnazimmoja. Taarifa zinaeleza kwamba kulikuwa na watoto takriban 30 na Watalii kutoka nchi mbali mbali wafikao kumi.
Wazamiaji kutoka Kikosi cha KMKM pamoja na Jeshi tayari wapo eneo la ajali kusaidia kuokoa maisha ya wananchi waliokumbwa na maafa haya.
Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250. Picha/Ramadhan Othman Ikulu
Toa Maoni Yako:
0 comments: