Madereva wametakiwa kuzingatia kanuni za usalama barabarani na misingi bora ya uendeshaji wa magari ili kuepuka ajali za mara kwa mara.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Kanda ya Ziwa ,ndugu Dede Petro alipokuwa akifunga mafunzo ya madereva wa abiria katika Chuo cha Mafunzo Stadi (VETA).

Alisema kuwa mafunzo waliyopata yawasaidie katika ubora wa kazi na kuzingatia sheria za barabarani. Aidha, ameongeza kuwa vyanzo vikuu vya ajali ni Madereva wengi kujifunzia mitaani hivyo hawajui taratibu na sheria za usalama barabarani.

Aliwataka Madereva hao wawe Mabalozi wa wengine na wawe chachu ya mafanikio kwani pato la Taifa linakua kutokana na mchango mkubwa unaotolewa na Madereva.

Sambamba na hayo, Bwana Dede aliwaasa Madereva kuungana pamoja kudai haki zao toka kwa waajiri wao ambao hawataki kuwapa mshahara badala yake wanatoa posho ya siku. Amewaomba madereva wabadilike waendane na mfumo uliopo, wasikubali manyanyaso toka kwa Waajiri.

Kwa upande wa risala ya Wahitimu hao wa mafunzo ya Udereva kwa Mgeni Rasmi ambao idadi yao ilikuwa sabini, walisema kuwa wamejifunza mambo mengi ya msingi yakiwemo jinsi ya kufuata misingi ya uendeshaji, namna ya kumhudumia abiria na jinsi ya kuepuka ajali.

Vile vile waliwaomba madereva waendeshao Pikipiki, nao wakapate mafunzo Chuoni hapo ili kuepuka ajali. Kwa pamoja waliiomba serikali huko waendako iwasimamie ili waweze kupata ajira na iweke mkakati wa kupunguza ada ili madereva wengi wakapate mafunzi VETA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: