“Mv Skagit ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 300 pamoja na mizigo tani 26,  hivyo kulingana na idadi ya abiria 288 walioondoka katika chombo hicho isingeweza kuleta madhara kama hayo, ila tunawasiwasi waliongeza abiria njiani au mawasiliano ya hali ya hewa” Kwa mujibu wa Meneja Mawasiliano David Mziray.

Kauli hii inaufanya umma wa watu ambao sasa ni waelewa kwa asilimia kubwa kuamini kuwa baadhi ya taasisi za serikali watendaji wake wanafanyakazi pasipo kujua wanafanya kazi gani.
a
Haiwezekani leo hii useme kuwa Boti ile inawezekana iliongeza abiria njiani...sasa wapi kuna gati huko baharini na hao abiria wanatokea wapi? ilhali safari ya boti kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar (Unguja) hakuna kituo hapo njiani. 

Lakini labda SUMATRA wana gati mpya Bagamoyo au Mbezi Beach huko. Ila hakika huu ni mtokoto wa mwaka 2012 na ni dharau kwa roho za watu na mali zao kwa mamlaka yenye dhamana ya kusimamiusafiri nchini. Habari/Mrokim Blog.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

4 comments:

  1. hiki ndo kilichosemwa kweli mbona kwenye magazeti sijaona haya?

    ReplyDelete
  2. hiki ndo kilichosemwa kweli mbona kwenye magazeti sijaona haya?

    ReplyDelete
  3. hiki ndo kilichosemwa kweli mbona kwenye magazeti sijaona haya?

    ReplyDelete
  4. hiki ndo kilichosemwa kweli mbona kwenye magazeti sijaona haya?

    ReplyDelete