Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Bw. Zelothe Stephen akiwaonyesha waandishi wa habari hawapo pichani vyeti feki vya watuhumiwa wa kundi la Matapeli la LAMBA LAMBA vyeti hivyo ni vya (UMAWATI )– cha mtuhumiwa DK. Shabani R Kisoma amacho kirefu chake ni UMOJA WA WAGANGA WATAFITI WA MAGONJWA SUGU UKIMWI NA TIBA ASILIA TANZANIA, na (CHAUMUTA) – Cha mtuhumiwa anayejiita DK. Hussein Shomari Mabogo, ambaye amekamatwa , kirefu chake ni CHAMA CHA UTAFITI WA MAGONJWA SUGU NA UKIMWI KWA TIBA ASILIA.
Baadhi ya watuhumiwa wa utapeli wa kufanya waganga wa kienyeji wa Kundi la Lamba Lamba wakiwa wameshika dhana za kazi wakiwaonyesha waandishi wa habari pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen hawapo pichani. Kutoka kushoto waliovaa kawaida ni Mkude S/O Mwenda 32 yrs, Mkulima, na Joseph S/O John miaka 27, Mkulima, wote wakazi wa Mkoka – Kongwa na SALEHE S/O OMARI, mwenye umri wa miaka26, mkulima wa Songe Kilindi Mkoani Tanga aliyevaa lubega nyekundu kwa nyeusi na ndani ana fulana mistari.
Watuhumiwa wa utapeli wa kujifanya Waganga wa Kienyeji na Tiba Asilia wa Kundi la Lamba Lamba wakiwa wameshika dhana za kazi, wakitekeleza amri ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen kuonyesha kile wanachowafanyia wanakijiji mbele ya waandishi wa habari pamoja na Kamanda huyo hawapo pichani. Picha/Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments: