Na Mwandishi Wetu

WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss dar Intercollege 2012 jumatano ya kesho wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Shindano hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo msanii wa bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kutumbuiza.

Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao watapata kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars "twanga Pepeta' kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila jumatano katika klabu hiyo.

Dina alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili kuweza kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa lengo la kujipoza baada ya mazoezi yao.

"Warembo wetu wamealikwa kesho pale Bilicanas ambapo bendi ya Twanga Pepeta hutumbhuiza kila Jumatano kupitia usiku wa Mwafrika, hivyo tunaoomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwashuhudia kabla ya kuja tena Ijumaa katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa,"Alisema

Alisema maandalizi ya shindano hilo yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaoshiriki wanaendelea na mazoezi katika hoteli ya The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam

“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.

Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.

Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Sporti Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Dinaismail(zamani Mamapipiro), Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: