Wakiwa wanamsikiliza Mwalimu darasani na wengine wakiandika kwenye madaftari ya mazoazi.
Wanafunzi wa shule ya msingi Etaro wakiwa darasani. Shule hii ipo wilaya ya Musoma vijijini.
---
UHABA wa madawati katika shule za msingi na sekondari umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla nchini, ikiwemo Shule za Wilaya ya Musoma Vijijini.

Upungufu wa madawati katika shule za msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya kusoma na mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.

Matokeo ya wanafunzi kukaa chini husababisha wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala kifudi fudi na wengine kuchuchumaa na hivyo kushindwa kuandika vizuri na pia kuchoka mapema. Hali hii kupelekea matokeo mabaya nyakati za mitihani hasa ya kitaifa.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Etaro wakiwa darasani wakimfuatilia mwalimu. wanafunzi wengi katika shule hii wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: