Taasisi ya African Trade Insurance Agency (ATI) ikiwa pamoja na Taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) leo zimezindua ‘Wiki ya ATI’ yenye lengo la kuhamasisha wadau kuhusu shughuli za ATI zinazotolewa kwa makampuni ya Tanzania.

ATI pamoja na TPSF zinalenga kuimarisha hali ya biashara hapa nchini ili kuweza kuvutia wawekezaji na biashara nyingi zaidi kwenye uchumi.

Tanzania kama mwanachama mwanzilishi na mwanahisa za ATI, imenufaika sana na huduma za taasisi hiyo, hivyo kuwa na ofisi nchini tangu mwaka 2010 ambapo ATI imefadhili zaidi ya Dola za Marekani bilioni moja za uwekezaji na biashara nchini kwa mwaka 2011.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara na majengo, ujenzi wa mitambo ya umeme na dhamana ya Dola za Marekani milioni 200 kwa miradi ya miundo mbinu iliyotolewa kwa serikali.

Taasisi ya African Trade Insurance Agency (ATI) ni taasisi ya aina yake inayoshughulikia bima za kifedha na dhamana, ambapo hufidia pale mnunuzi wa bidhaa za kampuni au mteja wake anatokea kutolipa au kulipa kwa muda ambao ni nje ya makubaliano.

Pia wakati kampuni inakabiliana na athari zitokanazo na serikali kusimamisha au kukwamisha biashara. ATI imejikita kutoa bima na dhamana dhidi ya athari zitokanazo na kutolipwa au na machafuko ya kisiasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: